Stevo Simple Boy: Sio kwa ubaya, KRG ni nani? Mbona tunapiganishwa kimuziki naye?

Wengi walihisi Stevo ni uchokozi ameanzisha dhidi ya KRG ambaye anatarajiwa kujibu mipigo vibaya sana.

Muhtasari

• Hata hivyo, wengi walihisi kwamba swali hili la Stevo linakaa balagha kwa kiasi kikubwa.

Stevo aanzisha vita na KRG
Stevo aanzisha vita na KRG
Image: Instagram

Msanii kutoka Kibera Stevo Simple Boy ameamuz kuanzisha ugomvi na vita ya kibabe baina yake na msanii mwenye mbwembwe nyingi KRG the Don kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Simple Boy alidai kwamba watu wengi wamekuwa wakimtaja KRG kwa ukurasa wake huku wakimlinganisha kimuziki na yeye, jambo ambalo limemfanya kuingiwa na uchu wa kutaka kumjua mtu huyo ni nani.

“Sio kwa ubaya ama nini, lakini huyu KRG ni nani nimetajwa sana kwenye Instagram, na mbona tunapiganishwa kimuziki?” Stevo Simple Boy aliuliza kwa kejeli.

Hii inakuja baada ya KRG kutoa wimbo mpya akimshirikisha Dufla Diligon na watu wengi kumtaja Stevo Simple  Boy kuwa wanaweza shirikiana kufanya muziki kutokana na kushabihiana katika staili zao za uimbaji.

Hata hivyo, wengi walihisi kwamba swali hili la Stevo linakaa balagha kwa kiasi kikubwa na kuwa alikuwa anatafuta vita vya maneno na msanii KRG ambaye hakawii kujibu mipigo.

Ikumbukwe wiki jana, Stevo alikanusha kuwa ngoma yake mpya ya Inabamba hakuimba wazo la video kutoka kwa video ya Khaligraph Jones, ngoma ya Kwame ambayo alimshirikisha Harmonize kutoka Tanzania.

Katika video hizo mbili, kufa mfanano mkubwa kwa jinsi video zimefanywa, lakini Simple Boy alisema kwamba mfanano huo haukutokana na kwamba alitaka kuiba wazo la Khaligraph bali ni kwa sababu pengine waongozaji wa video hizo zote walitoka Tanzania.