Diana B awarushia vijembe baadhi ya mastaa

Katika wimbo wake mpya,alionekana kuwalenga mastaa kadhaa.

Muhtasari

• Katika wimbo wake alisema kuwa Jimal Roho safi alirudi soko huku akisema kuwa pia Zuchu atarudi sokoni.

Mkewe msanii Bahati, Diana B,amewarushia vijembe mastaa Tanasha Dona, Zuchu na Amira akiwemo Andrew Kibe, katika kibao chake kipya "Narudi soko" akiwataja pia Amber Ray na Jimal akisema kuwa Amber Ray aligundua ulafi ndiposa akamwacha Jimal.

Katika wimbo wake alisema kuwa Jimal Roho safi alirudi soko huku akisema kuwa pia Zuchu atarudi sokoni.

"Kurudi  soko",ni neno ambalo limetumika na Wakenya kumaanisha hali ya kuwachwa.

Diana B pia alimlenga Andrew Kibe akimkashifu kwa kutusi watu ilhali yeye ni maskini, alimwambia kuwa atazikwa ghetto akifa. Katika kibao chake 'narudi soko',anadai kuwa hata baada ya kujifungua bado anang'aa huwezi jua kama amezaa.

Kwenye mtandao wa Youtube, Bahati alijibu akimuuliza ni soko gani anarudi ilhali yeye bado yupo, alimweleza atulie.

"Unarudi soko nikiwa wapi,hebu tulia wewe msichana," aliandika Bahati.

Diana B amekuwa akizozana na mwanablogu, Andrew Kibe huku Diana B akidai kuwa Andrew Kibe ni maskini. Diana aliongeza kuwa bila kutaja jina lake basi Andrew Kibe hana kazi.

Diana B pia aliuliza ni nani aliyeumiza roho ya Kibe kumfanya awe na machungu kiasi hicho. Aliweka picha ya Andrew Kibe na mpenzi wake wa zamani akisema kuwa inafaa mwanamke huyo atafutwe ili wamsihi arejee kwake Andrew Kibe

Kibe alimjibu Diana akisema mikataba ambayo Diana hupata ni kwa sababu ya Bahati kwa kuwa yeye hana jina .Alimweleza Bahati kuwa Diana si wa kawaida na kuwa kuna kitu anataka kufanya.