Jimal: Amira hakuniacha, mimi ndio nilimuacha! Amejaribu kuja kwangu mara 2 akafukuzwa!

"Alidanganya eti nilimpiga, mimi ni mkubwa sana kupiga mwanamke, AMira angekuwa amepigwa angekuwa amepakia hadi Ambulensi" - Jimal

Muhtasari

• Mbona amenifuata kwa nyumba yangu mara mbili akafukuzwa? Ni kitu cha kutumia akili - Jimal aliuliza.

Jamal asema hakuachwa na Amira bali yeye ndiye alimuacha
Jamal asema hakuachwa na Amira bali yeye ndiye alimuacha
Image: Instagram

Baada ya uvumi kuibuka mitandaoni kwa muda mrefu kwamba mfanyibiashara Jimal Rohosafi aliachwa na waliokuwa wapenzi wake wawili Amira na Amber Ray, sasa amejitokeza wazi kuzungumzia suala hilo.

Akizungumzia mazingira yaliyopelekea kuvunja uhusiano wake na aliyekuwa mke wake Amira, Jimal aliweka wazi kwamba kinyume na dhana zilizopo mitandaoni kuwa aliachwa, ukweli ni kwamba yeye ndiye alimuacha Amira na si kinyume chake.

Alifichua kwamba baada ya kumuacha, Amira alifanya jitihada za kujaribu kurudi nyumbani kwa Jimal mara mbili lakini akawa anazuiliwa, na kuwa hilo ndilo jambo linalompa hasira za kumzungumzia kwa mabaya mitandaoni.

“Ni mimi ndio nilimuandikia na nikasema asiwahi kanyaga kwa nyumba yangu. Mimi ndio nilimuacha na si yeye aliniacha kama anavyowadanganya kwa mitandao ya kijamii. Na kama yeye ndio angekuwa ananiacha hangekuwa anateta eti kwa nini sijampa hivi vitu vya nyumba? Mbona amenifuata kwa nyumba yangu mara mbili akafukuzwa? Ni kitu cha kutumia akili, kwa hiyo aache kudanganya watu huko nje…” Jimal alisema katika mahojiano na mwanablogu wa YouTube.

Mfanyibiashara huyo pia alitumia fursa kutoa ushauri kwa Amira akimwambia kwamba tayari yeye ameshajipa shughuli na maisha yake na katu hana haja ya ugomvi wa mitandaoni na yeye kuhusu ndoa yao iliyovunjika.

“Ushauri mmoja ninaoweza kumpa Amira ni kwamba mimi nilishasonga mbele na maisha. Tafadhali pia wacha kushinda ukinifuatilia kwa maisha yangu. Wewe umaarufu umeshawahi kuingia, ofisi yako ni Instagram, mimi siwezi kuzungumzia tena,” Jimal alisema.

Alisema kwamba kilichomfanya kumfukuza Amira kutoka kwa nyumba aliyomnunulia Syokimau ni baada ya kumpata akinywa pombe na sheesha katika nyumba hiyo, huku akikumbuka wakati mmoja kwamba aliwahi ambia kuna mwanamume amekuja kwa nyumba hiyo na gari la vitz.