"Usijaribu kujilinganisha na mtanashati kama mimi!" - KRG amjibu Stevo Simple Boy

Stevo SImple alianzisha vita vya maneno dhidi ya KRG akisema kwamba hamjui.

Muhtasari

• Jumatano, Stevo Simle Boy aliotesha ugomvi na KRG akisema kwamba hajui mtu anaitwa Krg na kutaka kujua ni kwa nini alikuwa anapiganishwa naye kimuziki.

Stevo aanzisha vita na KRG
Stevo aanzisha vita na KRG
Image: Instagram

Msanii KRG the Don amemjibu Stevo Simple Boy kufuatia matamshi yake kwamba hamtambu Krg ni nani.

KRG ambaye anaendelea kutamba kwa wimbo mpya aliomshirikisha Dufla Diligon aliibuka na jibu la kejeli dhidi ya Stevo akimuingilia kwa maumbile yake na kumtaka kutojaribu kujilinganisha naye hata kidogo.

Akizungumza kwa kebehi zake, KRG alisema kwamba Stevo Simple Boy kwake hatoshei hata kiganjani na kusema kwamba kile ambacho ataweza kumfanyia Simple Boy ni kumpeleka kwa shamba lake na kumpa kazi ya kutishia wanyama na ndege kwenye shamba lake

“Sasa wewe Stevo Simple Boy, chenye naweza kufanyia ni kukupeleka pale kwenye shamba langu, nikuvalishe kanga ukuwe kama kinyago. Kwa sababu sura yako inatisha sana, usijaribu kujilinganisha na mtu mtanashati kama mimi,” KRG alisema kwa dharau.

Jumatano, Stevo Simle Boy aliotesha ugomvi na KRG akisema kwamba hajui mtu anaitwa Krg na kutaka kujua ni kwa nini alikuwa anapiganishwa naye kimuziki.

“Sio kwa ubaya ama nini, lakini huyu KRG ni nani nimetajwa sana kwenye Instagram, na mbona tunapiganishwa kimuziki?” Stevo Simple Boy aliuliza kwa kejeli.

Tamko la KRG halikupokelewa kwa uzuri na baadhi ya wanamitandao ambao walimsuta KRG kwa kuingililia maumbile ya msanii huyo kutoka Kibera wakimwambia kwamba hakufaa kutumia hicho kigezo kumjibu Simple Boy.

Hata hivyo, wengine walihisi kwamba Simple Boy ndiye alianzisha vita vya maneno ambavyo hangeweza kuvimudu, huku sasa wakiwa wanasubiriwa jibu la msanii huyo kwake KRG.