Wakenya wanahukumu rahisi-Pritty Vishy asema kuhusu kifo cha Jeff

Kufuatia hilo, wapelelezi walitoa wito kwa umma kutoa taarifa yoyote ambayo itasaidia katika uchunguzi.

Muhtasari
  • Pritty amesema kwamba sio tabia njema kuhukumu, kwani baada ya mshukiwa wa mauaji ya Chiloba kupatikana kila mmoja alinyamaza.
Vishy atoa ujumbe kwa wanaume.
Vishy atoa ujumbe kwa wanaume.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Pritty Vishy amewashauri Wakenya wasubiri ukweli ujulikane kuhusu kifo cha Jeff Mwathi kuliko kuhukumu mapema.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Pritty alipeana mfano wa mauaji ya mwanaharakati wa LGBTQ Chiloba amabpo mengi yalisemwa na Wakenya kuhukumu watu tofauti.

Pritty amesema kwamba sio tabia njema kuhukumu, kwani baada ya mshukiwa wa mauaji ya Chiloba kupatikana kila mmoja alinyamaza.

"Kitu kimoja ambacho nimejifunza ni kuwa sisi Wakenya huwa tunahukumu haraka,tukiangalia nyuma kuhusu mauaji ya Chiloba kila mtu alikuwa anasema haki kwa Chiloba lakini baada ya mshukiwa mkuu kupatikana tulinyamaza

Sasa ni Jeff kila mtu anaongea kila mahali na kuhukumu, kwa nini msingoje ukweli ujulikane?kwa nini muhukumu? lakini mtasema kuwa sijui chochote,"Pritty Aliandika.

Matamshi yake yanajiri baada ya DCI kuanzisha uchunguzi wa kifo cha Jeff aliyefariki akiwa nyumbani mwa DJ Fatxo.

Kufuatia hilo, wapelelezi walitoa wito kwa umma kutoa taarifa yoyote ambayo itasaidia katika uchunguzi.

Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kindiki Kithure aliagiza mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, Mohamed Amin kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo..

“Kuhusu suala la marehemu Jeff Mwathi, tumezungumza na DCI Amin na kumwagiza atume kikosi cha wauaji kutoka makao makuu ya DCI kuchunguza kwa kina kisa hicho na kuchukua hatua zinazohitajika,” Kindiki alisema.

Waziri alithamini juhudi za wapelelezi hao katika kushughulikia suala hilo.