Ukitaka mwanamke wako akufirikie, mkope hela! - Nandy

Akili ya mwanamke huwaza sana mwanamume ambaye amemkopesha hela yake - Nandy.

Muhtasari

• “Ukitana mwanamke wako akufikirie kwa sana, mkope hela, atakuwaza sana huyo,” Nandy alishauri.

Nandy ashauri wanaume kuwakopa wanawake hela.
Nandy ashauri wanaume kuwakopa wanawake hela.
Image: Instagram

Nandy, msanii na bosi wa lebo ya wasanii wa kike pekee ya African Princess amewashauri wanaume njia nzuri jinsi ya kuziteka fikira na mawazo ya wanawake wao.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Nandy alishauri wanaume kwamba iwapo unataka kuwa wazo kuu katika kichwa cha mpenzi wako wa kike, basi una moja tu la kufanya ili kujinafasi kwenye fikira zake saa 24 za siku.

Mpenzi huyo wa msanii na mjasiriamali Billnass alishauri kwamba mwanamke yeyote ambaye amemkopesha mpenzi wake wa kiume hela, basi humfikiria kwa kiasi kikubwa kuliko mtu yeyote na kuwashauri wanaume kuwa na mazoea ya kuwakopesha wapenzi wao hela ili kupata kufikiriwa sana nao.

“Ukitana mwanamke wako akufikirie kwa sana, mkope hela, atakuwaza sana huyo,” Nandy alishauri.

Nandy ni mama wa mtoto mmoja ambaye hajawahi muonesha hata mara moja kwenye uso wa wanamitandao ya kijamii, jambo ambalo limekuwa likiwaaminisha wengi kuwa mtoto huyo huenda hayupo licha ya kuonekana na ujauzito mkubwa tu miezi kadhaa kuelekea kujifungua kwake.

Lakini hata hivyo, Nandy aliwahi nukuliwa akila yamini kwamba hakuwa na sababu yoyote ya kumtambulisha mwanawe kwenye mitandao ya kijamii, akisema kwamba atamlea hadi atakapokuwa mkubwa na kujifanyia uamuzi mwenyewe iwapo atajiunga na mitandao ya kijamii au la.

Siku chache zilizopita wakati wa kusherehekea siku ya wanawake duniani, mume wake Billnass alipakia picha ya pamoja ya Nandy na mama yake na kusema kwamba ndio watu wa karibu na roho yake na kudokeza kwamba katika picha hiyo mtu aliyekosa ni mtoto wake.

Lakini tukirudi kwa ushauri tata wa Nandy, je ni kweli kwamba mwanamke humfikiria sana mwanamume yule aliyemkopa hela zake?