Bahati ni baba ya mtoto wangu, si eti namkwamilia juu ni mume wa mtu - Yvete Obura

Obura alisema kwamba amekuwa na mpenzi Mkamba kwa zaidi ya miaka 2 na watu waache kusema kwamba amemkwamilia Bahati.

Muhtasari

• "Mimi sijamkwamilia Bahati, kwani si ni baba ya mtoto wangu sasa nitafanya?” Yvete Obura alisema.

• Vile vile aliwataka wafuasi na mashabiki wake wakome kueneza chuki baina yake na Diana Marua na pia kuwakanya wasimpe mzomo.

Yvette Obura azungumza madai ya Diana Marua kuwa ana roho mbaya
Yvette Obura azungumza madai ya Diana Marua kuwa ana roho mbaya
Image: Instagram

Takribani miezi miwili iliyopita, mwanablogu Diana Marua aliibua ukakasi uliopo baina yake na babymama wa mume wake Yvete Obura alipokuwa akimjibu shabiki mmoja aliyetaka kujua uwepo wa mtoto Mueni ambaye Bahati alipata na Yvete kabla ya kuchumbiana na Marua.

Katika jibu hilo, Marua alidokeza kwamba huenda kuna ugomvi wa chini kwa chini uliokuwa unaendelea baina yake na Obura, chanzo kikubwa kikiwa ni Bahati.

Marua alimtaja Obura kuwa mtu asiye na shukurani hata kidogo baada ya kukelewa mtoto na tangu hapo, wengi wamekuwa wakilisubiri jibu au tamko la Yvete Obura kuhusu madai hayo kwamba alimchukua mtoto wake Mueni kutoka kwa wengine.

Juzi, Obura alikuwa anashiriki kwenye kipindi cha maswali na majibu cha moja kwa moja mtandaoni Instagram na mwanadada mwingine na maswali yalikuwa mengi ambayo yalimtaka kuzungumzia sakata zima linalochemka baina yake na Bahati pamoja na Diana Marua.

Katika jibu lake, Yvete Obura aliwakemea wanaosema kwamba hata baada ya kuachana na Bahati, bado anamkwamilia mwanamuziki huyo, jambo ambalo alilikanusha vikali akisema kwamba kwa Zaidi ya miaka miwili sasa, anachumbiana na mpenzi mwingine na kile kinachompa ukaribu na Bahati pengine ni kutokana na uhalisia kwamab ndiye baba wa mtoto wake – Mueni.

“Mimi sichumbiani na Bahati, nina mpenzi wangu Mkamba na si Bahati pekee ndiye Mkamba. Na watu muache kusema kila siku eti nimekwamilia bwana ya wenyewe, Mungu wangu, mimi nimekuwa nikichumbiana kwa Zaidi ya miaka miwili. Mimi sijamkwamilia Bahati, kwani si ni baba ya mtoto wangu sasa nitafanya?” Yvete Obura aliuliza swali balagha.

Pia alikanusha kilichosemwa na Marua kwamba ana roho mbaya na kujipigia debe kwamba yeye ni mtu mzuri tu kwani akitaka kumzungumzia Marua watu watasema yeye ni mbaya na pia akiamua kunyamaza pia watu watazusha.

"Hata nyinyi mnajua kuna vitu huwa sizungumzii. Na nisipoongea mtasema niko na roho mbaya na nikinyamaza pia mtasema niko na roho mbaya," alisema.