RIP: Promota na Meneja wa zamani wa Aslay afariki dunia!

Babaz pia mpaka kifo chake alikuwa meneja wa kundi la ROSTAM ambalo lilikuwa linawajumuisha wasanii wa Hiphop Stamina na Roma.

Muhtasari

• “Babaz shukrani kwa mema yote, lala salama kiongozi,” Aslay alimuomboleza.

Aslay na wasanii wengine wakiwa na Babaz kipindi cha uhai wake.
Aslay na wasanii wengine wakiwa na Babaz kipindi cha uhai wake.
Image: Insatgram

Mdau wa muziki wa kizazi kipya kutoka ukanda wa pwani ya Kenya Mussa Babaz amefariki dunia.

Wengi wanamtambua Babaz kwa mchango wake mkubwa katika kukuza na kuwashika mkono vijana wengi waliokuwa wanaimba muziki wa Bongo Fleva hasa kutoka nchini Kenya na Tanzania pia kwa kiasi kikubwa.

Taarifa za kifo chake zilivujishwa mitandaoni na mtangazaji Mzazi Willy Tuva ambaye kwa kushirikiana na wasanii wengine wengi walimuomboleza Babaz kama mtu aliyejitolea pakubwa katika kukuza vipaji vya uimbaji katika mataifa haya mawili.

Una mchango mkubwa sana katika tasnia ya burudani. Umewashika mkono wasanii wengi tajika. Umekuwa rafiki na ndugu yangu. Tumekuwa familia moja. Tumefaana kwa mengi. Leo umetutoka na kutuachia majonzi makubwa. Nitabaki na kumbukumbu njema za wema wako. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un,” Mtangazaji huyo aliandika.

Babaz enzi za uhai wake, aliwahi fanya kazi ya kuwasimamia wasanii wa kufoka kama Stamina na Roma Mkatoliki kutoka kundi la Rostam, akafanya kazi na Aslay, Chege Chigunda, Jay Melody miongoni mwa wengine wengi.

“Babaz shukrani kwa mema yote, lala salama kiongozi,” Aslay alimuomboleza.

Nikisema niandike nitaandika vitu vingi sana,ila tu niseme imeniumiza mimi pamoja na familia yetu nzima ya ROSTAM!! Hukua BOSS tu kwetu,ulikua BABA kwenye shida na kwenye raha!! PUMZIKA KWA AMANI BABA YETU MUSSA BABAZ WA BABAZ😭 Ile simu ya juzi tunamtania @roma_zimbabwe ndio ilikua unaniaga kumbe!!daah nimeumia kwa kweli...” Stamina aliandika.