"Kwani hujui jokes!" Kevin Mboya apashwa kwa kudai Alinur hajampa ahadi ya 700K

Baada ya mpenzi wake kumtema alipomshtukia Kwale, Mboya alirudi Nairobi akilia na mwanasiasa huyo akaahidi kumfuta chozi kwa laki 7 na safari ya Dubai.

Muhtasari

• Takribani miezi 2 sasa, Mboya anadai kwamab bado hajapata kuona pesa hizo, hata hivyo hakudhibitisha kama safari ya Dubai ilifanikishwa.

•Watumizi wa Twitter walimpasha mwanablogu huyo wakimtaka kutotegemea kufanya vitimbi kama hivyo ili kuonewa huruma na kusaidiwa.

Mboya apashwa kwa kudai ahadi ya Alinur kama deni.
Mboya apashwa kwa kudai ahadi ya Alinur kama deni.
Image: Facebook

Kevin Mboya, mwanablogu ambaye aligonga vichwa vya habari mwezi Januari baada ya kudai kusafiri kutoka Nairobi kwenda Kwale kumshtukizia mpenzi wake, lakini ziara hiyo ikaenda fyongo.

Mboya ambaye baadae aliibuka na kusema kwamba mpenzi wake alimgeuka na kumsaliti kwa kumzimia simu na baada ya kimya cha siku kadhaa ambacho kiliwatia wasiwasi wanamitandao, Mboya alirudi akilia.

Watu wengi walimhurumia na mwanasiasa wa Nairobi, Alinur Mohamed alikuwa ni mmoja wa wale ambao walimhurumia na kujitolea kumfuta machozi.

Alinur kupitia kurasa zake mitandaoni, alijitolea kumpa shilingi laki 7 taslimu mwanablogu huyo pamoja pia na kufadhili safari yake ya wiki moja kwenda Dubai.

“Nilitabiri mambo hayatakwenda sawa kwa kijana huyu Kevin Mboya na baada ya kutazama video yake kwenye akaunti zake za kijamii, nimethibitisha hofu yangu. Hata hivyo yaliyopita si ndwele, namtafuta. Nitamlipia likizo yake ya wiki moja huko Dubai na kumpa KSH. 700k kwa matumizi yake,” Alinur alisema.

Hata hivyo, takribani miezi miwili baadae, Mboya ameibuka na jipya tena!

Anadai kwamba mwanasiasa huyo hakutii ahadi yake na mpaka sasa shilingi laki 7 alizomuahidi hajawahi kumpa hata shilingi moja hadi watu wanamuona wanadhani ako na pesa kufuatia ahadi hiyo.

“Ni mwezi mmoja, wiki mbili na siku mbili sasa tangu Mhe. Alinur alitoa ahadi hii. Bado hajaiheshimu. Kila mahali ninapoenda watu hufikiri nina pesa kwa vile wanaamini nina KSH. 700K. Kila siku ninaalikwa kwenye Harambee. Marafiki na jamaa zangu hunipigia simu kila siku kutaka kushiriki!” Mboya alilia.

Hata hivyo, baadhi walimkashifu kwa kudai kwa kifua ahadi ambayo mtu alimpa badala ya kusubiri na wengine wakimtaka kutafuta pesa zake mwenyewe na kuacha kufanya vitimbi ili kupewa ahadi za pesa.

"Tafuta pesa zako mwanamume wewe," mmoja alimwambia.

"Kwani hujui mzaha?" Mwingine alisema.