"Itakuwaje?" Harmonize akoshwa na tamaa baada ya kuona mzungu anaimba wimbo wake

Harmonize alisema kwamba yeye huwa hana uvivu anapoona rangi za wazungu na kuingiwa na mawazo ya kitakachotokea baina yao.

Muhtasari

• Kuonekana kumtamani kimapenzi mwanadada huyu kunakuja siku moja baada ya kumkaribisha mwanadada mwingine katika maisha yake kama mpenzi wake.

Harmonize amtamani mzungu
Harmonize amtamani mzungu
Image: Instagram

Msanii Harmonize kwa mara nyingine tena ameonesha kumtolea macho ya kumtamani mwanadada mmoja mwenye asili ya Wazungu ambaye alionekana akiimba wimbo wake wa ‘Single Again’ kwenye mtandao wa TikTok.

Harmonize alipakia video hiyo ya mwanadada huyo kwenye Instagram yake na kujidai kwamba kila mara anapoona sura kama hizi basi damu humchemka kwa kiasi kikubwa na kuwa huwa hana uvivu katika rangi za Wazungu.

Msanii huyo alionesha tamaa zake akisema kwamba kuiona sura hiyo tu kulimpa mawazo mtanange kuwa itakuwaje ikitokea nyota ya haja kuwa amekutana naye pap!

“Mimi sio mvivu sana na rangi hizi, nawaza tu itakuwaje?” Harmonize aliandika kwenye video hiyo ya mwanadada Mzungu.

 Mashabiki wake baadhi walimtaka kutojiingiza katika mtego mwingine tena na kumtaka kujichuna sikio kutokana na sakata la aliyekuwa mpenzi wake Muitaliano Sarah Michelotti ambaye mwaka jana amemburura kwenda mahakamani akidai sehemu ya mali ya msanii huyo.

 Hivi majuzi, baadhi ya media za Tanzania zilidai kwamba Sarah alishinda kesi hiyo ya kutaka sehemu ya mali za Harmonize kwani pia alikuwa mchangiaji mkubwa wa upatikanaji wa mali hizo, haswa kipindi ambacho Harmonize aliondoka WCB Wasafi ya Diamond kwa njia ya kishari mno na kuanzisha lebo yake ya Konde Music Worldwide.

Awali, Harmonize alikuwa amempuuzilia mbali Sarah kwamba hakuwahi mchangia kitu chochote na kudai kipindi hicho wakiwa katika uhusiano na Kajala kwamba ndiye alimpa hifadhi wakati hakuwa na kitu chochote.

Harmonize kuonesha kumtamani mwanadada huyu kunakuja siku moja tu baada ya kuonekana akimkaribisha mwanablogu Sishkiki Sikamatiki kwenye maisha yake akimtaja kama mpenzi wake.