Iran: Wasichana 5 wakamatwa wakicheza wimbo wa Rema 'Calm Down', Msanii avunja kimya!

Wasichana hao walionekana kwenye video wakicheza video ya wimbo huo wakiwa wamevalia nguo za kuonyesha tumbo zao, kinyume na sheria za Kiislamu wanawake kuvalia hijab

Muhtasari

• Katika Jamhuri ya Kiislamu, ni haramu kwa wanawake kucheza hadharani na vilevile kutovaa hijabu ya Kiislamu.

• Kukomeshwa kwa sheria ya hijabu imekuwa moja ya madai makuu ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe yaliyozuka Septemba mwaka jana,.

Rema atoa tamko baada ya wasichana wa Iran kukamatwa wakicheza video ya wimbo wake 'Calm Down'
Rema atoa tamko baada ya wasichana wa Iran kukamatwa wakicheza video ya wimbo wake 'Calm Down'
Image: Instagram, Twitter

Vijana watano wa Kiirani waliotamba na mwimbaji na rapa wa Afrobeat wa Nigeria, wimbo wa Rema ‘Calm Down’ wamedaiwa kukamatwa.

Video ya wasichana hao watano ilisambaa siku ya Jumanne kwa kucheza wimbo wa Rema bila hijabu – vazi maalum kwa ajili ya wanawake wa Kiislamu.

Picha zilionyesha wanawake wakicheza wimbo huo na kuonyesha matumbo yao kidogo, karibu na majengo ya miinuko katika wilaya ya makazi ya Tehran.

Video hiyo Ilienea sana kwenye TikTok na chaneli zingine za media za kijamii wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake mnamo Machi 8.

Kujibu tukio hilo, Rema alitumia Twitter kuelezea msukumo wake kutoka kwa wasichana na wanawake wengine wa Iran ambao wanapigania maisha bora ya baadaye.

Alitweet, "Kwa wanawake wote warembo wanaopigania ulimwengu bora, nimetiwa moyo na nyinyi, ninawaimbia, na ninaota nanyi."

Wanaharakati, wanaoonekana kutoka eneo la Ekbatan, walichapisha video hiyo kwanza kwenye Telegram na Twitter. Walisema mamlaka imekuwa ikiwauliza wakaazi katika eneo hilo ikiwa wanawafahamu wanawake hao, kulingana na picha, gazeti la Times of Israel lilisema.

Siku ya Jumanne, wanaharakati hao walidai wanawake hao walikuwa wamezuiliwa na kulazimishwa kutengeneza video ya kuwaonyesha wakijutia kitendo chao cha kucheza densi bila nguo za kiislamu na pia kuomba msamaha.

Katika Jamhuri ya Kiislamu, ni haramu kwa wanawake kucheza hadharani na vilevile kutovaa hijabu ya Kiislamu.

Kukomeshwa kwa sheria ya hijabu imekuwa moja ya madai makuu ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe yaliyozuka Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini, 22, ambaye alikuwa amekamatwa kwa madai ya kukiuka maadili ya mavazi.