logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mejja afichua kwa nini wanaume huteseka mikononi mwa warembo wakatili na hawaondoki

Mejja alisahuri wanaume kutoachia majukumu yao ya kawaida hata baada ya kuoa.

image
na Radio Jambo

Habari20 March 2023 - 06:53

Muhtasari


• Msanii huyo alisema wanawake wengi huchukua majukumu yote ya mwanamume wakati anaolewa na anapoondoka, mwanamume yule hushindwa kujizoa na kumbidi kumtafuta.

Mejja afichua sababu za wanaume kukwamilia wanawake warembo na wakatili.

Mwanamuziki wa genge wa muda mrefu, Mejja Okwonkwo amefichua sababu zinazowafanya wanaume kuteswa sana mikononi mwa wapenzi wao bila ya kutaka kuachia uhusiano huo.

Katika podikasti moja, Mejja alisimulia kutoka upande wake ni jinsi gani alipitia changamoto nyingi na kuteswa mikononi mwa mwanadada mmoja aliyekuwa mpenzi wake.

Mejja alisema kwamba wanaume wengi wanateswa mikononi mwa wanawake katili kwa sababu ya kugoma kufanya shughuli ambazo walikuwa wanafanya wakiwa singo, pindi wanapooa, wanaume hao huacha kufanya shughuli hizo na kuwategemea wanawake.

“Wanawake hao wakatili huwa wamemshika mwanamume katika shughuli hizi kidogo kidogo ambazo mwanamume anaweza fanya akiwa peke yake, mrembo huyo akiingia kwako anazichukua zote na kuzifanya, kipindi itatokea mmeachana ameondoka, unaanza kuteseka juu hujazoea kuzifanya, inabidi tena umeenda kumbembeleza…” msanii huyo alisema.

Msanii huyo pia alisema kwamba wanaume wengi huteseka mikononi mwa wanawake katili, kwa kuhadaika na umbile zuri la mwanamke huyo kiasi kwamba hata akikutesa bado utataka tu kurudi kwake kujifariji kwa kumuangalia muonekano mzuri wa kupendeza.

“Warembo wakatili huwa mara nyingi wamevia sana katika kupika na kila kitu. Hiyo ndio huwafanya wanaume wasiende mahali hata kama wanateswa. Unaambiwa tu na rafiki zako kwamba huyu mrembo anakutesa, unakubali ndio na pia unaona kuteswa huko lakini huwezi toka kwa sababu unamwangalia tu hivi alivyo vizuri unarudi kwake tena…” Mejja alisema.

Mejja alisahuri wanaume kuwa ukitaka kuanza maisha ya mwanamke, usiwahi kuacha kujifanyia vitu ambavyo ulikuwa unajifanyia ukiwa peke yako.

“Usipeane majukumu ambayo ulikuwa unafanya ukiwa peke yako. Haya majukumu madogo madogo ambayo unaachia mtu huwa yanakuchanganya na kukufanya ushindwe kujizoa wakati anaondoka, kwa sababu utakuwa unamkumbuka. Kama ulikuwa unajipikia mrembo akija, wewe endelea kujipikia, kwa sababu ile siku ataondoka, hayo majukumu madogo uliachia huanza kukuumiza kutekeleza,” alishauri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved