Pritty Vishy aahidiwa 600K kuigiza video za kufanya mapenzi, atakubali au atakakaa?

Vishy alisema kwamba hamjui mtu huyo ambaye amekuwa akitumia namba tofauti kumtafuta akimuahidi kazi hiyo.

Muhtasari

• "Kusema kweli, imekuwa zaidi ya miezi 5 kupata vile kwenye WhatsApp yangu. Hata mimi niko salama kweli?” - Vishy.

Vishy aahidiwa kazi ya kuigiza video chafu, akataa
Vishy aahidiwa kazi ya kuigiza video chafu, akataa
Image: Instagram

Mwanablogu Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy amefichua kwamba anafuatwa na watu wasiojulikana wanataka kumpa kandarasi ya kushiriki katika kutengeneza video chafu za kushiriki mapenzi.

Vishy alishiriki mtandaoni kwamba amekuwa akipata maombi kama hayo katika ujumbe wake wa simu na kupitia mtandao wa WhatsApp kwa miezi mitano iliyopita.

"Jinsi ninavyopata DM na kupigiwa simu zisizojulikana nikiambiwana  watu wanaoniambia niende kukutana nao mahali fulani ili kuigiza video za kushiriki mapenzi. Nikiwazuia watatafuta namba nyingine. Ninaogopa hata sasa. Kusema kweli, imekuwa zaidi ya miezi 5 kupata vile kwenye WhatsApp yangu. Hata mimi niko salama kweli?” Vishy alisema.

Vishy aliendelea kushiriki picha ya skrini ya mazungumzo yake na mmoja wa watu waliotaka kumwajiri kuigiza video hizo. Mtu huyo alidai kuwa Vishy atalipwa Kshs 600,000 ili kuigiza, akiongeza kuwa hakuna mtu atakayejua ni yeye.

Hata hivyo hakupendezwa na mpango huo.

"Hapana, sina nia," alisema.

Mwajiri huyo aliuliza zaidi ikiwa ana nia ya kufanya mahusiano ambayo yangemfanya apate Kshs50,000 kwa saa tatu, akiongeza kuwa walikuwa wakitafuta wanawake wanene tu.

Wiki kadhaa zilizopita, Vishy alidokeza kwamba alikuwa anataka mwanamume ambaye anaweza kumhudumia akisema kwamba hakuwa amepata mpenzi baada ya kutengana na mwanamuziki Stevo Simple Boy mapema mwaka jana.

Vishy amekuwa akiorodhesha viwango na hadhi ya ya wanaume ambao angependa kuwapa nafasi katika maisha yake, akionekana kulenga wale walio na mifuko minene yenye vina virefu.