logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi ni kijana mwenye roho safi sana, msiangalie sura - Stevo Simple Boy

Stevo alisisitiza kwamba anawapenda sana mashabiki wake wanaompa shavu.

image
na Radio Jambo

Makala28 March 2023 - 10:26

Muhtasari


• "Apana angalia sura angalia roho kijana roho safi,” Stevo alisema.

• Chapisho lake linakuja siku kadhaa baada ya kudhihakiwa vibaya na msanii wa dancehall KRG The Don.

Msanii Stevo Simple Boy asema ana roho safi hata kama sura si nzuri.

Rapa Stevo Simple Boy amewashauri mashabiki wake kutomhukumu kwa sura yake akisema kuwa ana roho safi.

Stevo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikejeliwa mitandaoni kutokana na maumbile yake haswa sura alisisitiza kwamba ni wakati watu waangalie roho au moyo badala ya kuishia kwa sura tu.

Msanii huyo kutoka mtaa wa mabanda wa Kibera alipakia video inayomuonesha ikiwa na wimbo aina ya Rhumba ambapo kwa kiasi aliandika kwa lugha ya Kifaransa na kutafsiri kwamba anapenda mashabiki wake wanaomkubali bila vigezo vyovyote.

Papa matulinga Papa kamirigado papa malovidovi.. J'aime mes fans (yani napenda mashabiki Sana) Apana angalia sura angalia roho kijana roho safi,” Stevo Simple Boy alishauri.

Chapisho lake linakuja siku kadhaa baada ya kudhihakiwa vibaya na msanii wa dancehall KRG The Don. Krg alimshukia Stevo baada ya rapper huyo kudai kuwa hajui yeye ni nani na haelewi kwanini alikuwa akilinganishwa mitandaoni na yeye.

Akimjibu, Krg alisema kuwa kazi pekee anayoweza kumpa Stevo ni kumfanya mtu wa kuogofya na kutisha minyama wanaoharibu mimea shambani.

“Wewe ni mtoto mdogo, wewe ni mnyama mdogo sana mbele ya macho yangu. Wew mimi nikilinganisha ile kazi naeza kupa wewe simple boy, labda nikupeleke kwa shamba langu uko nikuvalishe khanga kama scarecrow, kwa sababu sura yako inatisha sana. Usijaribu kabisa kijana. Sura yako inatisha sana kujilinganisha wewe na mtu mtanashati kama mimi. Wewe unakaa kama scarecrow ile kitu imechukuliwa kama tikiti maji uitobolee mashimo tu mianya,” KRG alisema maneno hayo ya dhihaka ambayo hata hivyo hayakuwafurahisha wengi wa watumizi wa mitandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved