Akothee, Jaguar, Sauti Sol kwenye 10 bora ya wasanii matajiri Afrika Mashariki

Orodha hiyo ilitawaliwa na wasanii wa kiume huku Akothee akiwa msanii wa kike pekee kujipenyeza katikati yao.

Muhtasari

• Orodha hiyo ilitawaliwa pakubwa na wasanii wa kiume, Akothee akiwa wa kike pekee katika kumi bora.

Forbes watoa orodha mpya ya wasanii matajiri Afrika Mashariki.
Forbes watoa orodha mpya ya wasanii matajiri Afrika Mashariki.
Image: Instagram

Kila mwaka, jarida la Forbes hutoa orodha ya watu wa vitengo na tasnia mbalimbali na kulinganisha utajiri wao.

Mwaka 2023, Forbes wametoa orodha ya wasanii matajiri kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, na kufuta uvumi na tetesi ambazo zimekuwa ziliwekwa kuhusu wasanii wa ukanda huu na utajiri wao katika tasnia ya muziki.

Orodha hiyo ilitawaliwa pakubwa na wasanii wa kiume, Akothee akiwa wa kike pekee katika kumi bora.

Msanii aliyegeuka kuwa mwanasiasa kutoka Uganda, Bobi Wine ndiye msanii tajiri kabisa katika ukanda wa Afrika Mashariki akiwa na utajiri wa dola za Kimarekani milioni 9.

Nafasi ya pili anakuja mfalme wa miziki ya kizazi kipya kutoka Tanzania Diamond  Platnumz ambaye utajiri wake kutoka kwa biashara zake za vyombo vya habari, lebo na kampuni ya ubashiri vyote vinajumuisha dola za Kimarekani milioni 8.2.

Mkongwe wa muziki Jose Chameleone anaibuka katika nafasi ya tatu akifuatiwa na Akothee wa Kenya, Professor Jay, Alikiba wote wa Tanzania kisha mwanasiasa Jaguar wa Kenya.

Msanii ambaye hana miaka mingi kwenye muziki, Harmonize amejipambania katika nafasi ya nane akifuatiwa na bendi ya muda mrefu kutoka Kenya, Sauti Sol na Bebe Cool wa Uganda anafunga 10 bora.

Hii hapa orodha rasmi na utajiri katika dola za Kimarekani pamoja na uraia wa wasanii hao.

  1. Bobi Wine (Uganda) na Dola milioni 9
  2. Diamond Platinumz (Tanzania) na Dola milioni 8.2
  3. Jose Chameleon (Uganda) na Dola milioni 8.
  4. Akothee (Kenya) na Dola milioni 7.6
  5. Professor Jay (Tanzania) na Dola milioni 7.5.
  6. Ali Kiba (Tanzania) na Dola milioni 7.2.
  7. Jaguar (Kenya) na Dola milioni 7.
  8. Harmonize (Tanzania) na Dola milioni 5.9.
  9. Sauti Sol (Kenya) na Dola milioni 5.8.
  10. Bebe Cool (Uganda) na Dola milioni 5.62