Amber Ray aonesha matumaini makubwa kurudiana na Jimal siku moja huku mbeleni

Amber Ray na Jimal wamekuwa wakioneshana heshima na hisia za kimapenzi hata baada ya kuachana takribani miaka miwili iliyopita.

Muhtasari

• "Lakini acha tusubiri tuone kesho yetu inatuandalia nini,” Ray alijibu swali hilo kuhusu kutoka kimapenzi na Jimal huku mbeleni.

Amber Ray na Jimal Rohosafi
Amber Ray na Jimal Rohosafi
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Amber Ray bado hajafutilia mbali kabisa matumaini ya siku moja kuja kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, mfanyibiashara Jimal Rohosafi.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye instastories zake, shabiki mmoja alimuuliza Ray kama bado wanachumbiana na Jimal licha ya kuwa na ujauzito unaodhaniwa kuwa wa Kennedy Rapudo, Ray alisema hawachumbiani lakini akadokeza kwamba huwezi jua kesho itakuwaje, akiashiria kwamba bado hisia za Jimal bado zipo.

“Kule kuchoka nimechoka siwezi jishuhulisha na kitu chochote mpaka nizae. Lakini acha tusubiri tuone kesho yetu inatuandalia nini,” Ray alijibu swali hilo kuhusu kutoka kimapenzi na Jimal huku mbeleni.

Jibu hilo linakuja saa chache tu baada ya Kupakia picha ya gari jipya aina ya Range Rover akisema kuwa ni zawadi ambayo Jimal, mpenzi wake wa zamani alimpa kama kumpoza baada ya kudai uhusiano wake na babake kijacho Kennedy Rapudo umevunjika.

Ray ni mjamzito kwa sasa hivi na mimba anayo ni ya Rapudo, lakini mapema wiki hii, wawili hao waliweka wazi mitandaoni kwamba wameamua kuachana bila hata kutoa sababu kwa mashemeji wa mitandaoni.

Hata hivyo, Rapudo alidokeza kwamba kuachana kwao huenda kuaambatana na sababu ya mimba hiyo, akisema kwamba anasubiria miezi miwili mtoto azaliwe ndio ajue mbivu na mbichi – kunyoa au kusuka!

Lakini alinyoosha maelezo baadae kuwa hakuwa na maana ya kushuku ujauzito huo iwapo ni wake na kusema ako tayari kulea mtoto huyo kwa namna yoyote ile.

Kwa upande mwingine, Jimal hata baada ya kudokeza kuwa na mpenzi mpya hivi majuzi, bado amekuwa akionekana kumkubali sana Amber Ray n ahata kumpa sifa kedekede wakati wa kumlinganisha na mke wake wa kwanza, Amira.

Jimal aliwahi nukuliwa akisema kwamba Amber Ray ni mtu mzuri lakini aliyekuwa mbaya katika uhusiano wao ni Amira, na kumsifia huko kunarudi palepale kwamba watu hao wawili siku moja watarudiana tu!