logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Sisi ni manusura!" Esther Musila awashauri wanarika wake kutojiskia vibaya kwa kuzeeka

Musila aliwashauri wanarika wake kufurahia kila sekunde ya maisha yao.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri08 April 2023 - 05:44

Muhtasari


•Musila alibainisha kuwa kufikia umri mkubwa wa zaidi ya miaka 40  ni fursa maalum ambayo sio watu wengi hupata kufurahia.

• Ndoa ya Guardian Angel na Esther Musila imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na tofauti kubwa ya umri wao. 

Mkewe Guardian Angel, Bi Esther Musila amewataka wanawake wenye umri wa miaka 40-60 kuthamini hatua muhimu  waliyofikia maishani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watatu wakubwa alibainisha kuwa kufikia umri mkubwa wa zaidi ya miaka 40  ni fursa maalum ambayo sio watu wengi hupata kufurahia.

Kwa sababu hiyo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 53 amewataka wanarika wenzake  wasijisikie vibaya kuhusu uzee wao.

"Hata kama miili yetu haiwezi kuwa kama ilivyokuwa hapo awali, inabeba roho zetu, ujasiri wetu, na nguvu zetu. Hatupaswi kamwe kujisikia vibaya kuhusu uzee. Ni upendeleo ambao umenyimwa kwa wengi," alisema siku ya Ijumaa.

Musila aliwashauri wanarika wake kufurahia kila sekunde ya maisha yao.

Alibainisha kuwa wanawake wa rika lake wamepitia mengi maishani na kuna mabadiliko mengi yanayotokea katika miili yao kadri umri wao unavyosonga mbele. Kufuatia hayo, aliwataja kama mashujaa kwa kushinda mengi maishani.

"Tuko katika umri huo ambapo tunapata makunyanzi usoni, mvi na uzito zaidi. Tumetunza boma, tumelipa bili, tumeshughulikia magonjwa, huzuni, na kila kitu kingine ambacho maisha yametupangia. Sisi ni manusura, sisi ni wapiganaji katika utulivu, sisi ni Wanawake, kama gari la kawaida au divai nzuri," alisema.

Musila, 53, alifunga pingu za maisha na mwanamuziki Peter Omwaka almaarufu Guardian Angel, 33, mapema mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa muda. Ndoa yao hata hivyo imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na tofauti kubwa ya umri wao. Hata hivyo, baadhi wamewapongeza kwa kushinda kanuni za kijamii.

Kabla ya kuolewa na Guardian Angel mwaka jana, Bi Musila alikuwa kwenye ndoa nyingine na hata kubarikiwa na watoto watatu. Mumewe wa kwanza hata hivyo aliaga dunia takriban miaka saba iliyopita.

Mwezi Machi 2020 ndipo alipokutana na mwimbaji huyo wa nyimbo za injili na kuchumbiana naye kabla ya kufunga ndoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved