Msanii Bahati amemshukuru mke wake Diana B kwa kuwa mama bora kwa watoto wake na kwa kumuunga mkono kila wakati.
Katika chapisho alilopakia Diana B kwenye mtandao wa Instagram, Bahati kupitia Whatsapp alieleza shukrani zake na kummiminia sifa Diana akisema watoto wake walipata mama bora zaidi duniani.
Bahati aliongezea kuwa ana furaha kila wakati anapomuona Diana B akiwa na furaha.
"Mpenzi,niko hapa nakufikiria na nikiwaza jinsi wanangu walipata mama bora zaidi duniani, na jinsi dunia yangu sio ya kawaida bila wewe, nataka tu kukukumbusha kuwa wewe ni wangu milele na nitafanya kila niwezalo kukufanya uwe na furaha," alisema Bahati.
Bahati aliongezea kueleza kuwa anatamani kuona wakizeeka pamoja,alimshukuru Diana kwa kumtunza na kumchunga mwanao Malaika huku akieleza furaha yake kwa kuwa katika maisha yake.
Kwa upande wake Diana, alifurahishwa na ujumbe wa mume wake naye akimshukuru mumewe kwa kumpenda kila wakati na kumwamini yeye.
"Asante kwa kuniamini kuwa ndani ya safari ya maisha yako,asante kwa kuwa amani yangu, nguvu yangu, utulivu wangu na furaha yangu. Nina furaha kufanya hili na wewe kila siku, nakupenda," ,alisema Diana.
"Maneno ya uhakikisho, penzi ni jambo zuri," alijibu Milly Chebby, mkewe mcheshi Terence.
Hivi majuzi, mtoto wao, Malaika Bahati alikuwa mgonjwa na kulazwa hospitalini kwa siku saba sasa. Diana na Bahati wamekuwa hospitalini wakimshughulikia kuwa na matuamaini ya yeye kuwa mzima.