DJ Pierra Makena asherehekea kufikisha miaka 42, watu hawaamini

Wengi walimtania kwamba amejiongezea miaka na kusema kwamba umri wake sahihi huenda ni chini ya miaka 25.

Muhtasari

• “Hii miaka yako unakuanga umeficha wapi...Siu zote mbichi...Kheri njema Zaidi ya kuzaliwa mrembo,” Sharon Amadala aliuliza.

• Makena ambaye mi mama wa binti mmoja hajawahi dokeza waziwazi mahusiano yake mitandaoni.

DJ Pierra Makena asherehekea miaka 42
DJ Pierra Makena asherehekea miaka 42
Image: INSTAGRAM

Mcheza santuri wa kike wa muda mrefu Pierra Makena Jumanne alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufichua kwamba alirauka akiwa amefikisha miaka 42.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makena, mama wa binti mmoja alipakia picha akiwa amevalia nguo ya manjano akiwa amewaka kwa tabasamu na kinyume na wengi wanaoficha kutangaza umri wao, Makena alisema kwamba amefikisha miaka 42.

“Niliamka leo nikiwa nimefikisha miaka 42,” Makena aliandika.

Hata hivyo, wengi wa mashabiki wake walionekana kutoamini umri wake, wakisema kwamba DJ huyo pengine anadanganya kwa kujiongezea umri, kwani kwa jinsi alivyo anaonekana mdogo na mbichi sana kufikisha miaka 40 na ushee.

“42 ndio umri mpya wa 24 weh😍 happy birthday,” Sophie Diana alisema.

Hii miaka yako unakuanga umeficha wapi...Siu zote mbichi...Kheri njema Zaidi ya kuzaliwa mrembo,” Sharon Amadala aliuliza.

Miezi miwili iliyopita, DJ Pierra Makena aligonga vichwa vya habari baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na mkuza maudhui wa TikTok mwenye umri wa miaka 23, Creative Phil.

TikToker na msanii huyo wa kujipodoa anadaiwa kuwa mpenzi wake mpya baada ya kuweka picha akiwa na Makena wakionekana kuwa na mahaba.

Picha yake ilifuatiwa na picha iliyowekwa na Makena akiwa amevalia gauni lililodokeza kuwa ilikuwa siku ya harusi yake; mama wa mtoto mmoja huwa hachapishi kuhusu mahusiano yake.

Wanamtandao wamemfananisha na Musila na sosholaiti wa Uganda Zari Hassan, ambao wote wanajulikana kwa kuchumbiana na wanaume wenye umri mdogo kuliko wao.

"Mumama to the world!!!!! Mama wa Gwagon!! @creativephill ungependa gari gani kwa Valentines toto!" Pierra Makena alimuuliza Phil katika chapisho hilo.