Mchekeshaji mwenye uwezo tofauti amepokea mchango mkubwa wa Naira milioni moja ambazo ni sawa na shilingi 292K za Kenya kutoka kwa Peter Okoye maarufu Mr P wa kundi la wanamuziki la PSquare, katika kile alisema ni tuzo ya kumfurahisha.
Peter alifurahishwa na utendaji bora wa mcheshi huyo chipukizi na mlemavu katika tamasha la mchekeshaji AY Live, toleo la hadithi yake, ambalo alihudhuria kipindi cha pasaka.
Baada ya mchekeshaji huyo kilema kupanda jukwaani na kusisimua umati kwa ucheshi wake, Mr P aliendelea kutambua nia yake ya kumzawadia naira milioni moja na pia alitoa wito chapa nyingine kubwa na watumbuizaji kusaidia mcheshi huyo chipukizi.
Mr P alifurahishwa na ucheshi wa kijana huyo pamoja na ukakamavu na ujasiri wake kuweza kuvuka vikwazo vyote vya ulemavu na kusimama mbele ya mamia ya watu kuwachekesha.
“Mimi binafsi nitakupa Naira milioni moja. Kabla sijaendelea nani anaungana na mimi kumsaidia huyu kijana? Haijalishi unafanya nini, tumpe msaada tu. Kaka nakukubali sana. Nimekuja kutoka huko nyuma hadi hapa mbele ili kukuona ukichekesha, kwa sababu ucheshi huo ulininasa sana,” Mr P anaonekana kwenye jukwaa akimwambia kijana huyo.
Onyesho la vicheshi lililopendwa sana lililoandaliwa na Ay lilipata uwepo wa wajasiriamali matajiri, watumbuizaji, na watu binafsi wenye thamani ya juu.
Wasanii wa kundi la PSquare Mr P na Rudeboy ambao ni mapacha walivuma siku za nyuma kabla ya kutengana na kurudi pamoja tena miezi kadhaa iliyopita ambapo tena wameanza kuvuma.
Wiki chache zilizopita baada ya kukamilika kwa uchaguzi nchini Nigeria, wawili hao walikwenda zao Ughaibuni kila mmoja akiwa na nia ya kununua makaazi ya kifahari huko.
Mmoja wao alinunua nyumba Atlanta nchini Marekani huku mwingine akidokeza kununua jumba Lojdon Uingereza.