logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ringtone: Nampenda sana Akothee, nilikuwa napanga kumuoa!

Ringtone alimwandikia Akothee hundi ya 999k kama zawadi ya harusi yake,.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 April 2023 - 05:24

Muhtasari


• Baada ya kumuandikia Akothee hundi ya 99k, alisema kuwa Kenya yeye na KRG ndio mabilionea wasanii pekee.

• Ringtone alisema sababu ya kutoenda kwa harusi hiyo ni kuwa hakungekuwa na nafasi ya kutua na helikopta maana Butita alishafika pia na helikpta.

Ringtone asema anampenda sana Akothee, amwandikia hundi ya 999k.

Msanii wa injili mwenye vituko, vimbwanga na utata mwingi, Alex Apoko maarufu kama Ringtone anadai kwamba alikuwa na mpango wa kumuoa mwanamuziki Akothee na kufunga harusi na yeye.

Ringtone ambaye muda mwingi maneno yake huchukuliwa kwa mzaha na utani alisema kuwa anampenda sana mjasiriamali huyo wa Akothee Safaris na alikuwa na mipango mingi sana ya kumfanya mke halali endapo angekosa mwanamke wa kuoa.

Kapera hiyo alimwandikia Akothee hundi ya karibia milioni moja, akisema kuwa ni zawadi ya harusi yake ambayo hakuhudhuria.

“Esther Akoth nimemwandikia hundi ya 999k, mimi nampenda sana Akothee, na ingefika siku moja, nilikuwa napanga nikikosa mtu wa kuoa nimuoe Akothee. Ako tu mtu mzuri sana na mimi napenda wanawake viherehere, mradi tu kiherehere chake kinanipeleka kwa Mungu,” Ringtone alisema.

Hata hivyo, Ringtone alisema kuwa hakupewa mwaliko katika harusi hiyo licha ya mapenzi yake mengi kwake.

Ringtone alisisitiza kwamba Akothee hakuolewa bali ndiye alimuoa Omoshi, mzungu kutoka Uswidi, huku pia akisema kuwa mzungu huyo atakuwa anatumiwa kufanya kazi za ndani kwa Akothee.

“Akothee hakuolewa, alioa. Yule hawezi olewa. Na Omosh akicheza anapigwa, akikataa kufanya kazai za ndani atapigwa. Pale Omosh pengine alipenda Akothee lakini hakumjua vizuri, pale kupigwa nako atapigwa sana. Lakini asiogope kusema maana sisi ndio tutamtetea,” Ringtone alisema.

Msanii huyo wa injili mwenye majigambo mengi alijitapa kuwa angeingia kwenye harusi ya Akothee basi helikopta zingekuwa nyingi na nafasi ya kutua ingekosekana.

Msanii huyo alisema kuwa katika Sanaa ya Kenya, wasanii mabilionea ni wawili tu, akisema ni yeye na msanii mwingine wa kujitapa sana, KRG the Don - na ndio matajiri hawakualikwa kwenye harusi hiyo, akiwapuuzilia mbali wasanii wengine walioalikwa kuwa ni "watu wa njaa".


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved