logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini sikuhudhuria harusi ya Akothee-MCA Tricky

Mchekeshaji huyo alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya harusi ya Julai 10,

image

Burudani14 April 2023 - 12:35

Muhtasari


  • Tricky alisema kuwa hakuona sababu ya kuhudhuria harusi hiyo, kwa sababu ni miongoni mwa waliochaguliwa ambao watakuwa na Akothee nchini Uswizi.

Mchekeshaji maarufu nchini MCA Tricky hatimaye amejitokeza wazi kufichua sababu, kwa nini hakuhudhuria harusi ya Akothee.

Tricky alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotarajiwa kujitokeza kwenye harusi hiyo, lakini cha kushangaza, mchekeshaji huyo hakuonekana popote Akothee alipokuwa akifunga pingu za maisha na mumewe.     

Akizungumza kwenye mahojiano na 2mbili tv, MCA Tricky ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa Rue Baby, alisema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asijitokeze kwenye harusi ya wakwe zake, ni kwa sababu yuko kwenye orodha ya watu watakaokwenda Uswizi. .

Tricky alisema kuwa hakuona sababu ya kuhudhuria harusi hiyo, kwa sababu ni miongoni mwa waliochaguliwa ambao watakuwa na Akothee nchini Uswizi.

Aliwataka watu kuacha kuwaza kupita kiasi, kwa sababu alikuwa na nafasi ya kujitokeza, lakini walikubaliana kwa pamoja na Akothee kuwa ataenda kwa harusi ijayo.

Mchekeshaji huyo alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya harusi ya Julai 10, na hatawakatisha tamaa Wakenya, atajitokeza akiwa amepambwa vyema na atawawakilisha vyema huko nje.

Akuzungumza kuhusu uhusiano wake na Rue Baby, kwa ujumla alisema kwamba yeye na Akothee wana uhusiano mzuri, na ilikuwa ni mapenzi yake tu kutohudhuria harusi ya Kenya, bali kuhudhuria ile ya Uswizi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved