logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Naacha muziki na kuingia katika mchezo wa kupigana ngumi - Willy Paul

Pozee amekuwa akishiriki picha na video akinyanyua vyuma kwenye gym.

image
na Radio Jambo

Habari14 April 2023 - 07:59

Muhtasari


• Iwapo ataacha muziki kwenda mieleka, basi itakuwa mara yake ya pili kuacha alichokuwa akikifanya, kwani alivuka hivo hivo pia kutoka injili kwenda sekula.

Willy Paul adai kuacha muziki na kwenda boxing.

Msanii na mkurugenzi mkuu wa lebo ya Saldido International, Willy Paul ametangaza kuwa yuko tayari kuacha muziki na kujitosa mazima katika mchezo wa kupigana ngumi.

Msanii huyo ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akitisha mitandaoni kwa kupakia picha na video zikimuonesha akijibiisha katika mazoezi ya kunyanyua vyuma aliyasema haya baada ya kuona kuwa misuli ya mwili wake imetuna sawasawa na mtu anayeshiriki mieleka.

“Naacha muziki na kuanza mchezo wa mieleka,” Willy Paul alitangaza baada ya kupakia picha moja akiwa ametunisha misuli.

Hata hivyo, Pozee ambaye si mgeni kwa kiki alizua fikira kutoka kwa baadhi ambao walihisi kuwa ni sehemu ya video ya muziki ambayo anaiandaa akiwa anashiriki mazoezi ya kunyanyua vyuma, na wengine kumtakia mema katika safari ya mabadiliko mengine.

Kwit basi bado utarudi tu kwa muziki.....sababu muziki  kwako ni kama nyumbani,” mmoja alisema.

“Safi, upige ule jamaa wa tz anaitwa nani,,,, @madonga_mtu_kazi alale wiki mzima,” mwingine alimtania.

“Na muda wote  tunatarajia uwe kidedea.. Mabondia wa Kenya ni sharti wawe juu kupitia kwako Pozee,” huyu naye alimtia moyo.

Ikubukwe msanii huyo pia alianza kwa utani tu hivi akisema kuwa angehama tasnia ya miziki ya injili na kuingia miziki ya kidunia.

Hata hivyo, baada ya kugura injili na kujijengea ufuasi mkubwa kwenye miziki ya sekula, Pozee alipata mapokezi makubwa yaliyofuatwa na mafanikio kimuziki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved