Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Wasafi Diamond Platnumz kwa mara nyingine tena amesisitiza watoto wa kiume kwamba kuna haja na kutafuta pesa kwanza kabla ya mapenzi.
Hata hivyo, Simba, kama anavyojiita, amesema kuwa kupata pesa na utajiri si njia mwafaka ya kutarajia mapenzi ya kweli, akidai kuwa kuna changamoto nyingi katka upata penzi la kweli ukiwa unanukia utajiri.
“Pindi tu baada ya kuwa tajiri, kila msichana utakayekutana naye atataka pesa zako na wala sio mapenzi yake ya kweli,” Platnumz alisema.
Platnumz anahisi kwamba wanawake ni viumbe wa ajabu sana ambao kuwaelewa ni kibarua cha kujaribu kupasua jabali ili kupata maji.
Msanii huyo anayetajwa kuwa namba mbili ukanda wa Afrka Mashariki katika utajiri, kulingana na orodha ya Forbes ya mwaka huu alisema kwamba mwanamke ni mtu unayeweza kujitoa kwake kwa asilimia mia ukimfanyia kila kitu lakini mwisho wa siku ukikwamba kidogo tu kifedha, basi ndio naye anakupiga teke.
“Mfanyie mambo Zaidi ya milioni, ya kumfurahisha. Lakini sasa wewe pata tatizo la mkwamo kidogo kifedha, atakuonesha rangi za tabia yake halisi,” Diamond alisema.
Hata hivyo, msanii huyo alisisitiza kuwa watu watafute hela akisema kuwa maisha ya kisasa huwezi kufanikisha jambo lolote pasi na pesa.
Diamond katika siku za hivi karibuni amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kuonekana kanisani siku ya Pasaka, wakati wengi wanamjua kama Muislamu anayefunga mwezi mtukufu wa Ramadhan.