Mama Dangote adokeza Diamond amemwandikia mali yake yote, "Ni Hakimi"

Mama Diamond alidokeza kuwa mtoto wake ni kama Hakimi ambaye alimrithisha Mali yake yote mama yake.

Muhtasari

• Bado swali linalozidi kutawala mitandaoni ni je, ni vizuri mwanamume kumuandikishia mali yake mama yake na mke wake akiwa ?

• Kwa kumalizia na jina Hakimi moja kwa moja inaleta tafsiri kwamba ni mali ya mwana kuandikishwa kwa mama yote.

Mama Dangote adokeza kumiliki mali yote ya Diamond.
Mama Dangote adokeza kumiliki mali yote ya Diamond.
Image: Instagram

Bi Sandra au Mama Dangote amezua gumzo mitandaoni baada ya kudokeza kuwa mwanawe, Diamond Platnumz amemwandikishia mali yake yote chini ya jina lake.

Mama Dangote kupitia Instagram yake alipakia picha ya pamja wakiwa wamekumbatiana na mwanawe Diamond kwa tabasamu kuu na kuweka kapsheni inayodokeza kuwa mali ya Diamond yote yako chini ya jina lake.

Ki vipi?

Mama Dangote alidokeza hili kwa kutumia falsafa ya mchezaji wa Morocco na klabu ya PSG, Achraf Hakimi ambaye amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa siku tatu sasa baada ya uvumi kuibuka kuwa alikuwa ameandikishia mali yake yote kwa jina la mama yake.

Best yangu wa ukweli 💙 Naseeb kichwa @diamondplatnumz 🦁 Hakimi,” Mama Dangote aliandika.

Kwa kumalizia na jina Hakimi moja kwa moja inaleta tafsiri kwamba ni mali ya mwana kuandikishwa kwa mama yote.

Hakimi alisemekana kuandikisha mali yake yote kwa jina la mama yake wakati mke wake aipochukua kesi ya kutaka talaka akidai pia kupewa Zaidi ya nusu ya mali ya mumewe.

Kwa mshangao mkubwa, mahakama ilidaiwa kubainisha kwamba mchezaji huyo hakuwa na mali hata kidogo, urithi wake mwingi ukiwa chini ya miliki ya mama yake mzazi.

Mtandaoni, makundi yamekuwa yakihasimiana kufuatia uamuzi wa Hakimi kumpa mama yake mali yake, wavulana wakifurahi na kusema kuwa mchezaji huyo ndio himizo lao huku kina dada wakisimama upande wa mke wa Hakimi kwa hakumfanyia msichana wa watu vizuri ikizingatiwa wana watoto wawili pamoja.

Bado swali linalozidi kutawala mitandaoni ni je, ni vizuri mwanamume kumuandikishia mali yake mama yake na mke wake akiwa ?