Nililipwa milioni ya kwanza nikiwa na miaka 17 na nilimpa mamangu pesa hizo zote! - Rema

Msanii huyo maarufu kwa kibao cha "Calm Down" aliyazungumza haya huku kukiwa na gumzo pevu kuhusu sakata la talaka ya Hakimi na mkewe.

Muhtasari

• Mwimbaji huyo wa Calm Down alisema mafanikio yake makubwa ni kuweza kuhudumia familia yake na kutengeneza fursa kwa wengine.

Rema adokeza pesa zake za kwanza alimpa mamake zote.
Rema adokeza pesa zake za kwanza alimpa mamake zote.
Image: Instagram

Nyota wa muziki wa Afrobeat wa Nigeria, Divine Ikubor, maarufu kwa jina la Rema, amefichua kuwa alitengeneza naira milioni moja akiwa na umri wa miaka 17 na kumkabidhi mama yake pesa zote.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 alifichua haya katika mahojiano ya hivi majuzi na Z100 New York.

"Mtu ambaye nilijua alihitaji zaidi alikuwa mama yangu. Kwa hiyo, nilimkabidhi kila kitu nilichotengeneza. Najua ni ndoto ya kila mtu kuendesha gari la kifahari kama kijana wa miaka 17 katika mizunguko ya jijini. Lakini siwezi kuendesha gari zuri wakati mama yangu hakuwa na gari au mama yangu lazima aazime funguo zangu ili kutumia gari. Unajua, ilibidi nimsitiri kwanza,” alisema.

"Kumpa yote hayo, uwekezaji wowote anaofanya ... nilipata milioni yangu ya kwanza [naira] nikiwa na umri wa miaka 17 lakini nilipata zaidi ya milioni moja. Lakini ni vizuri kuwa katika hatua hiyo kuweza kuhudumia familia yako.”

Akizungumza zaidi, mwimbaji huyo wa Calm Down alisema mafanikio yake makubwa ni kuweza kuhudumia familia yake na kutengeneza fursa kwa wengine.

“Mtu fulani alinitengenezea fursa ya kubariki ulimwengu kiasi hiki. Kwa hivyo, siwezi kufikiria ni kiasi gani watu niliowasaidia wataubariki ulimwengu. Unajua, mimi huenda kwa bidii si kwa ajili yangu tu. Ninaenda kwa bidii kwa ajili yao. Milango inapofunguliwa kwangu, nataka kuwafungulia milango watu pia,” aliongeza.

Tamko la msanii huyo linakuja kipindi ambapo kina mjadala mzito mitandaoni kuhusu ni nani mwanamume anafaa kuandikia mali yake ya urithi kati ya mamake na mke wake.

Gumzo hilo lilizaliwa baada ya uvumi kuibuka kwamba mchezaji wa PSG na timu ya taifa ya Morocco Hakimi Achraf alimwandikia mamake mali zote na si mke wake.

Hilo lilibainishwa baada ya mkewe kufika mahakamani akitaka kumtaliki mchezaji huyo huku akidai zaidi ya asimilia 50 ya mirathi.

Kwa kushangazwa, mahakama ilibaini kwamba msanii huyo alikuwa amefilisika huku mali zake zote zikiwa chini ya mkanda wa mama yake.