logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msimu wa pili wa filamu ya uhalisia ya Young, Famous & African kuanza Mei

Katika msimu wa pili, sura mpya takriban vijana 5 wanajumuishwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 April 2023 - 05:44

Muhtasari


  • • Young, Famous & African ni mfululizo maarufu wa uhalisia wa Afrika Kusini ulioonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye Netflix mnamo Machi 2022.
Zari Hassan na Diamond Platnumz

Kampuni ya filamu ya Netflix hatimaye imetangaza tarehe ya kuachiliwa kwa msimu wa pili wa filamu ya uhalisia ya Young, Famous & African.

Kwa hivyo ikiwa unatarajia kutazama msimu mpya kabisa, hakikisha unaendelea kusoma ili kujua maelezo yote muhimu.

Young, Famous & African ni mfululizo maarufu wa uhalisia wa Afrika Kusini ulioonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye Netflix mnamo Machi 2022.

Unafuata maisha ya kikundi cha vijana, watu mashuhuri na matajiri wa 'media' wengi wao wanaoishi Johannesburg, Afrika Kusini.

Watazamaji hutazama kundi la marafiki wanapojenga taaluma zao, kutafuta mapenzi na wakati mwingine ugomvi.

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu kwa miezi kadhaa, mtayarishaji mwenza wa filamu hiyo Peace Hyde alitangaza kwamba kipindi hicho kingerudi kwa msimu wa pili kupitia chapisho la Instagram.

Lakini kwa kuwa Netflix haijawahi kutoa tangazo rasmi la kusasisha, mashabiki wa kipindi walikuwa na wasiwasi kwamba Young, Famous & African msimu wa 2 haingetolewa.

Lakini si kweli, kwani Jumanne Netlfix kupitia ukurasa wa Instagram wa Netflixsa walitangaza kuwa msimu wa pili umekamilisha na ni muda tu kuanza kutazamwa kwenye runinga.

Msimu wa pili wa mfululizo wa uhalisia unatarajia kutua kwenye Netflix mnamo Ijumaa, Mei 19, 2023. Jumla ya hesabu ya vipindi haijulikani kwa sasa, lakini pengine tunaweza kutarajia vipindi vingine saba kama vile msimu wa kwanza.

Waigizaji waliorejea ni Andile Ncube, Annie Macaulay-Idibia, Nadia Nakai, Naked DJ, Zari Hassan, Khanyi Mbau, Swanky Jerry, Kayleigh Schwark, Diamond Platnumz, na 2Baba.

Hata hivyo, msimu wa pili utaona nyuso na sura mpya wakiwemo:

Bonang Matheba - Mtangazaji na mwigizaji wa televisheni aliyeshinda tuzo kutoka Afrika Kusini.

Fantana - Mwanamuziki wa Afro-Dancehall mwenye asili ya Ghana na Marekani.

Luis Munana - Mshiriki wa zamani wa Big Brother Africa na sasa ni mtayarishaji wa TV, mwandishi, na mkurugenzi wa ubunifu.

Sebabatso Mothibi - Mwanamitindo na msosholaiti.

Rosette Ncwana - Rosette ni mwanamitindo mkuu na mwigizaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved