logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dadake Diamond kupendana na Harmonize si jambo geni - DJ wa Harmonize afichua

“Siwezi kumchagulia. Mimi Konde Boy akiwa na yeyoote tu ni shemeji yanu, tunaondoka tu, yeyote! "

image
na Radio Jambo

Habari28 April 2023 - 05:48

Muhtasari


• Harmonize alidai kwamba Esma alishiriki katika wimbo huo, na hata wawili hao kuzua uwezekano wa kuonana kinyemela.

DJ Seven afunguka ishu ya Harmonize na Esma Platnumz.

DJ Seven, ambaye ni mwandani wa karibu sana wa msanii Harmonize amefunguka kuhusu sekeseke za mitandaoni ambazo zinamhusisha msanii huyo na Esma Platnumz, dadake Diamond.

Uvumi wa Harmonize kutoka kimapenzi na dadake Diamond umekuwa ukigonga vichwa vya habari kwa Zaidi ya wiki moja sasa, haswa baada ya DJ Seven kutoa wimbo wa ‘Say Yes’ ambao alimshirikisha Harmonize.

Harmonize alidai kwamba Esma alishiriki katika wimbo huo, na hata wawili hao kuzua uwezekano wa kuonana kinyemela.

Suala la Harmonize kutoka kimapenzi na Esma ni kubwa ikizingatiwa kwamba Harmonize na Diamond walishavunja ukuruba wao muda mrefu tu na nusra wazichape.

Sasa wakati wa mahojaino na vyombo vya habari kutambulisha albamu yake, DJ Seven ambaye ana ukaribu mkubwa na Harmonize aliulizwa kuhusu suala la rafiki yake kutoka kimapenzi na dada wa adui yake kimuziki.

Seven alisema kuwa suala hilo si la ajabu kwani ni sawa tu Harmonize akimpenda mtu yeyote ni kawaida na sawa tu na wataondoka naye kwenda Marekani kufanya video ya ngoma hiyo yake.

“Siwezi kumchagulia. Mimi Konde Boy akiwa na yeyoote tu ni shemeji yanu, tunaondoka tu, yeyote! Mimi kwangu ni sawa tu awe Esma, awe Kajala anarudi, Wolper au Sarah sina tatizo,” DJ Seven alisema.

DJ Seven alifichua kwamba katika ziara yake ya Marekani ambapo ataongozana na Harmonize, moja ya dhima ni kufanya video ya collabo ya ‘Say Yes’ ambayo vile vile alidokeza kwamba gharama zote zitasimamiwa na Harmonize licha ya kuwa ngoma hiyo ni ya DJ Seven.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved