logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Brownskin avunja kimya wiki 3 baada ya video ya mkewe akinywa sumu kuibuka

Brownskin alidokeza kwamba watu wanaamini uongo na kuwa huenda ana hadithi ya kusimulia.

image
na Radio Jambo

Makala30 April 2023 - 06:39

Muhtasari


• Brownskin alidokeza kwamba huenda naye pia ana hadithi ya kusimulia kwa upande wake kuhusu video hiyo.

• Baba mkwe wake alisema kuwa Brownskin alimdanganya kuhusu matukio yaliyojiri siku ya kifo cha bintiye.

DJ Brownskin katika mazishi ya mke wake.

Wiki kadhaa baada ya kukashifiwa na umma kwa kumtazama mpenzi wake Sharon Njeri akitumia kile kilichoaminika kuwa sumu na baadaye kufa, Michael Macharia almaarufu DJ Brownskin amevunja ukimya wake.

Kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambalo ni la kwanza tangu video hiyo iliposambaa mitandaoni, Brownskin alionekana kupendekeza kwamba kuna Zaidi ya kile ambacho watu waliona na ghafla kuanza kumhukumu pasi na kujua kiini cha kila kitu kilichojiri.

Brownskin alipakia ujumbe ambao kwa asilimia kubwa ulionekana kuwalenga wale waliodakia mitandaoni kwa kumkashifu kwa kuwa na roho mbaya kumtazama aliyekuwa mpenzi wake akibugia sumu na kufa mbele ya watoto wake pasi na kuonekana kuchukua dharura yoyote.Alishiriki nukuu, "Mtu yeyote anayeamini uongo kukuhusu kabla ya kusikia upande wako wa hadithi alikuwa tayari anatafuta njia ya kuwa dhidi yako," akidokeza kwamba ana hadithi ya kusimulia.

Mtandaoni, wengi walimlaumu Brownskin kwa kurekodi mkewe Sharon akibugia sumu na hata baba mkwe wake, Albert Mwangi, alisema ni unyama kwake kufanya hivyo.

Baba mkwe katika mahojiano ambayo alifanya siku chache baada ya video hiyo kuibuka mitandaoni, aliema kuwa Brownskin alimpigia simu mwaka jana wakati bintiye alikunywa sumu akimtaarifu kuwa alikuwa amewapeleka watoto shuleni na kurudi akampata Sharon amefariki kwa sumu.

Hata hivyo, baba mkwe alihisi kusalitiwa na taarifa ya awali kutoka kwa Brownskin kwani video hiyo iliyoibuka ilionesha tofauti na maelezo yake awali – Brownskin alikuwepo mkewe akinywa sumu.

“DJ Brownskin aliniambia kuwa alikuwa amewapeleka watoto shuleni na aliporudi akakuta Sharon amekunywa sumu. Video niliyoona inaonyesha kitu tofauti kabisa kwa sababu nadhani ndiye aliyerekodi binti yangu alipokuwa akipigania maisha yake," alisema.

“Alinidanganya na tangu video hiyo itokee hatujazungumza. Yeye (Brownskin) anajua alinidanganya.”

 Kipindi hicho chote, Brownskin alikaa kimya na hata akafikia wakati mmoja akaweka akaunti yake ya Instagram kuwa binafsi kabisa kiasi kwamba hakuna mtu nje ya wale wanqaomfuata angeweza kuona kilichomo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved