logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Davido atoa jibu la kishuzi kwa shabiki aliyemuuliza Chioma alienda wapi

Wasanii wengi aghalabu huwa hawajibu maswali lakini ikifika ni yale ya kughasi hupiga msumari.

image
na Radio Jambo

Habari29 April 2023 - 11:50

Muhtasari


• Shabiki huyo alitaka kujua mke wa Davido, Chioma aliko.

Davido aongoza kweney chati za muziki za UK France na Kanada.

Si kawaida kwa watu maarufu mitandao kujibu maswali au vitu ambavyo mashabiki wao huwauliza katika upande wa kutoa komenti.

Lakini mara moja moja tu huwa tunawaona baadhi ya watu hao maarufu haswa wasanii wakijibu baadhi ya vitu ambavyo mashabiki wao huuliza.

Lakini mara nyingi pia tunawaona wengi wa wasanii waqkijibu vikali kama nji ya kumkaba mtu ambaye anauliza kitu cha kuhasi.

Sasa juzi kati msanii Davido alimpiga kumbo shabiki mmoja kwenye mtandao wa Instagram ambaye aliuliza swali la kizushi kutaka kujua mbona msanii huyo siku hizi haonekani kwenye picha na mkewe Chioma Rowland.

Davido ambaye si mwepesi wa kujibu, safari hii ni kama alikuwa na muda mwingi tu kwenye mtandao wake wa Instagram ambapo alitoa jibu la kishuzi pia katika swali la aina hiyo, na kuwaacha wengi wa watumizi wa Instagram wakiwa katika kicheko cha kukata maini.

Shabiki huyo alitaka kujua iwapo Chioma alitoroka nyumbani, jambo ambalo huenda lilihusiana na masuala ya sasa ambayo Davido anayo na Chioma kwa madai kwamba amemuweka mwanamke mwingine kwenye njia ya familia baada ya kuachana hivi karibuni.

Davido alimfahamisha shabiki huyo kupitia Instagram kuwa Chioma yuko kwa mumewe.

“Yuko wapi Chioma?” Adjoa the Promoter aliuliza.

“Yuko nyumbani kwa mumewe,” Davido alijibu mipigo.

Katika taarifa inayoambatana na hiyo, Radio Jambo awali tuliripoti jinsi gavana wa Nakuru Susan Kihika aliwapiga misumari mikali kichwani baadhi ya watumizi wa Twitter amabo walijaribu kumuingia ngozini.

Kihika alimjibu vikali mmoja aliyemzomea kwamba atakuwa tu gavana wa muhula mmoja na hatoshinda katika uchaguzi wa 2027. Katika jibu lake, Kihika alimuuliza kwa upole japo kwa kishuzi kuwa yeye anayezidi kubweka mitandaoni ni mihula mingapi amewahi ongoza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved