Kwa nini Kim Kardashian anataka kustaafu usosholaiti na kuwa wakili na mwanaharakati?

Kim Kardashian bado si mwanasheria rasmi lakini anatumai kuwa juhudi zake katika harakati za kisheria zitakuwa "kazi yake ya maana zaidi maishani."

Muhtasari

• "Kila mara mimi hutania mama yangu - ambaye ni meneja wangu - nasema Kim K. anastaafu, na mimi nitakuwa tu wakili." - Kim alisema.

• Kazi ya mageuzi ya Kim ilianza Oktoba 2017 baada ya kujifunza kuhusu kesi ya dada mmoja aliyekuwa gerezani tangu Oktoba 1996.

Kim Kardashian atathmini kuacha usosholaiti na kuwa wakili.
Kim Kardashian atathmini kuacha usosholaiti na kuwa wakili.
Image: Instagram

Mashabiki wake kote ulimwenguni hawawezi kufikiria showbiz bila Kim Kardashian lakini nyota huyo wa vipindi vya uhalisia kwenye runinga hakika anaweza.

 Kim hivi majuzi alifichua mustakabali wake katika vuguvugu la mageuzi ya haki ya jinai alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa TIME100.

Kim alidokeza kwamba anatathmnini kuachia mbali kufanya vipindi vya uhalisia kwenye TV na kujitupa muda wote katika masuala ya kisheria.

"Ningefurahi vile vile kuwa wakili wakati wote," alijibu alipoulizwa ikiwa angewahi kufikiria maisha bila kutazamwa runingani. "Safari hiyo ilinifungua macho sana," alishiriki, na kuongeza, "Inakuwa nzito kwa sababu kuna mengi ya kufanywa ... nilimleta dada yangu Khloe (Kardashian) gerezani kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, na hilo lilimfungua macho sana.”

Kim Kardashian bado si mwanasheria rasmi lakini nyota ya Keeping Up With The Kardashian alimwambia mtangazaji Poppy Harlow kwamba anatumai kuwa juhudi zake katika harakati za kisheria zitakuwa "kazi yake ya maana zaidi maishani."

"Natumai hivyo," alisema, na kuongeza, "Kila mara mimi hutania mama yangu - ambaye ni meneja wangu - nasema Kim K. anastaafu, na mimi nitakuwa tu wakili."

Kazi ya mageuzi ya Kim ilianza Oktoba 2017 baada ya kujifunza kuhusu kesi ya Alice Marie Johnson, ambaye alikuwa gerezani tangu Oktoba 1996 baada ya kuhukumiwa kwa kusaidia kuwezesha mawasiliano katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya.

Alijitolea wakati wake kumwachilia Johnson na hata alikutana na Rais wa zamani Donald Trump juu ya suala hilo. Trump alibadili hukumu yake mwaka wa 2018 na Johnson akaachiliwa.

Tangu wakati huo, Kim ameendelea kutetea kuachiliwa kwa wafungwa wengine kadhaa na akafichua mnamo 2019 kwamba alikuwa akisomea kuwa wakili.