logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto wa Nandy na Billnass ajiendesha kuingia kanisani kwa ubatizo wake

Wote walikuwa wamepambwa kwa mavazi meupe kuonesha utukufu.

image
na Radio Jambo

Habari02 May 2023 - 05:07

Muhtasari


• Mtoto huyo alizaliwa mwaka jana na ana takribani umri wa miezi saba hivi.

• Wenzi hao walihakikisha kuwa ulikuwa ni mkusanyiko mdogo wa familia na marafiki zao. Ukumbi uliopambwa kwa uzuri unaonyesha ladha ya Nandy

Billnass na Nandy wakiwa katika tukio la ubatizo wa mwanao.

Wikendi iliyopita wasanii Nandy na Billnass walisherehekea hatua nyingine muhimu kama wazazi baada ya kushuhudia ubatizo wa mwanawe wa kike.

Wawili hao walikuwa wamevalia mavazi ya rangi nyeupe wakiingia kanisani ambapo Nandy alisherehekea na kwa mara ya kwanza kutaja kuwa mwanawe ni binti.

Katika video ambayo Nandy aliipakia, mwanawe huyo japo hakufichuliwa sura yake alionekana akiwa ameketi juu ya kigari chake cha mdoli akijiendesha kuingia kanisani kwa shughuli yake kubwa.

Jana ilikuwa siku ya kipekee na kiroho kwa binti yetu! Ameweza kutimiza agano la MUNGU LA KUBATIZWA.. inatupasa kumlea mtoto kwa njia impasayo MUNGU basi na MUNGU ametupa kibali cha kusimama madhabahuni kwake na kutimiza agano lake jina lake lihimidiwe 🙏🏻.. Shukrani kwa wana familia wote waliijumuika na sisi jamaa na marafiki MUNGU AWABARIKI SANA,” Nandy aliandika.

Katika tukio zima hilo, wanandoa hao walikuwa makini kwa kiasi kikubwa kuificha sura ya mwanawe, kama njia moja ya kutimiza nadhiri ambayo waliitoa hata kabla ya mtoto huyo kuzaliwa kwamba hawangemuonesha hata kidogo mitandaoni.

Mtoto huyo alizaliwa mwaka jana na ana takribani umri wa miezi saba hivi.

Wenzi hao walihakikisha kuwa ulikuwa ni mkusanyiko mdogo wa familia na marafiki zao. Ukumbi uliopambwa kwa uzuri unaonyesha ladha ya Nandy

Miongoni mwa walioalikwa ni Rayvanny na mpenziwe Fayhvanny pamoja na mtoto wao Jayden. Rayvanny alishinda sifa za mashabiki kwa kuweka familia yake pamoja.

Billnass naye alimsifu Rayvanny kwa kuunga mkono hafla ya ubatizo.

"Ahsante sana vanny boy na familia ya chui shemeji yangu, mmefanya usiku wa mtoto wangu kuwa aina yake..siku zote familia kwanza.."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved