logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Stevo Simple Boy hatimaye azindua juisi yake ya Freshi Barida

Msanii huyo pia alitangaza kuzindua kinywaji kingine kwa jina chaser.

image
na Radio Jambo

Habari02 May 2023 - 06:53

Muhtasari


• “Vitu vizuri vinachukua muda lakini wakati umekaribia wa kuburudika na freshi barida utamu wa kinywaji" - Stevo.

Msanii kutika Kibera, Stevo imple Boy

Rapa wa kizazi kipya kutoka Kibera Stevo Simple Boy hattimaye ametimiza ndoto yake ya muda mrefu kwa kuzindua kampuni yake ya kutengeneza juisi kwa jina Freshi Barida.

Stevo alitangaza hilo mwaka jana baada ya wimbo wake wa Freshi Barida kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake na kauli ya ‘Freshi Barida’ kukumbatiwa na wengi kwa ucheshi na mbwembwe.

Stevo amesema kwamba mpaka sasa asilimia tisini na tisa ya kila kitu kimekamilika na ni muda mchache tu umesalia ili juisi hiyo iweze kuingizwa sokoni kwa ajili ya matumizi.

“Vitu vizuri vinachukua muda lakini wakati umekaribia wa kuburudika na freshi barida utamu wa kinywaji (sampuli), hivi karibuni tunazindua. Muda unayoyoma jitayarishe kunywa juisi ya freshi barida na kinywaji cha kuongeza nguvu cha chaser,” Steve alidokeza.

Miezi tisa iliyopita, msanii huyo alifichua azma lake hilo kwa mara ya kwanza na kusema kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kujishughulisha kwenye biashara kando na muziki.

Akiandika kupitia Instagram yake, Simple Boy alidokeza kwamba hivi karibuni Mungu akimjaalia kinywaji hicho kitakuwa madukani.

“Na Mungu akituzidia zitakuwa madukani hivi karibuni tukuwe freshi barida,” aliandika staa huyo aliyetamba na kutambulika na wengi kwa wimbo wake wa kwanza wa ‘Mihadarati’


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved