Nairobi hakuna polisi rafiki yako, ni rahisi kukamatwa hata uwe nani - Chebet Rono

Mle ndani hakukuwa na maji kwa hivyo ilikuwa ni suala la uvumilivu na kuvuta harufu ya hicho choo," - Ronoh

Muhtasari

• Mashambulizi yake yalikuwa yanawalenga aliodai walimwibia maudhui yake ya, " Aunty Debs." 

Chebet Ronoh aliyekuwa mtangazaji amefunguka kuwa siku ya jumamosi alikamatwa na kulala korokoroni. chebet alisema, " kwa masaa kumi na moja nililala sakafuni na nilichopitia na hiyo baridi ni mungu tu anayejua."

Isitoshe Ronoh aliongeza kwa kusema kuwa ni rahisi sana kukamatwa katika kaunti ya Nairobi kwani ni alijikuta katika mazingira sahihi kwa wakati usiofaa. Anaendelea kwa kuelezea kuwa kama umewahifikiria kuwa unawezabishana na afisa wa polisi huku Kenya basi  ni lazima uwe mwendawazimu kwa kuwa afisa yule ataichukua kama madharau kisha akupeleke korokoroni.

Mwanablogu yule anasema," afisa yule alimweka pingu rafiki yake Chebet naye alipojaribu kumtetea rafiki yake basi bila yeye kujua gari la afisa lilikuwa limesimama mbele yake likimkaribisha ndani.mwanzoni kila kitu kilikuwa cha kuchekesha lakini tukifika kituoni hakuna kilichokuwa kichekesho sio tabasamu.

"Nlikuwa nimevaa shati na suruali. Baridi ilianza kupenya kwenye mifupa yangu na sikuwa na soksi. Mle ndani tulikuwa watu wawili  kuta nne na choo. Mle ndani  hakukuwa na maji kwa hivyo ilikuwa ni suala la uvumilivu na kuvuta harufu ya hicho choo,"Ronoh alisema.

Rono ambaye ni mtangazaji wa zamani wa kituo kimoja humu nchini aliongezea kuwa  wakati nafsi yake kukubali kilichotokea alianza kuimba nyimbo za ukombozi inayosema Paulo na Silas nakuambia hicho kiatu kivue." Anasema kuwa  walikuwa wakipiga utani lakini kila kitu kilikuwa kigumu na aliiishia kula chakula chochote ili kupata joto.

Ronoh anadai,"ningeweza kufanya lolote ili nitoke hapo."

Miezi kadhaa iliyopita mwanablogu huyo wa YouTube alivuka mipaka na kwanza kuwashambulia wenzake akiwemo muigizaji Kate Actress, mtangazaji Kamene Goro  na wachekeshaji Cartoon Comedian na Elsa Majimbo aliyeko Marekani.

Mashambulizi yake yalikuwa yanawalenga aliodai walimwibia maudhui yake ya, " Aunty Debs" 

Hili lilizua ukakasi mwingi mitandaoni baadhi wakimtetea kwa kupigania maudhui yake huku wengine wakimsuta vikali wakisema kwamba huenda hakuwa katika hali sawa ya kiakili.

Ronoh siku chache zilizofuata kupitia ukurasa wake wa Twitter alitoa tamko la kuomba radhi akisema kwamba alipata ndoto ya kumkanya kutoendeleza mashambulizi dhidi ya marafiki zake kwenye kitivo cha ukuzaji maudhui.