Mwanamziki maarufu wa muziki ya Muguthi DJ Faxto amejitokeza kwa umma kwa mara ya kwanza baada ya uchunguzi wa kifo cha Jeff Mwathi kukamilika.
Mwathi, 23, alikufa mnamo Februari 22, 2023 baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 10 ya jengo analoishi DJ Fatxo.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Fatxo alitangaza kurejea kwake akisema yeye ni kama ndege iitwayo Phoenix, ambayo hupepea licha ya changamoto zinazotupwa njiani pake.
"Na kama vile Phoenix alipoinuka kutoka kwenye majivu, nitasimama pia!” Faxto alisema.
Faxto ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi majuzi aliwasihi wakenya kumuombea akisema kuwa mwaka wa 2023 umekua mgumu kwake.
“Kurudi kutoka kwa miale ya moto, bila kuvikwa chochote ila nguvu na ushindi wa ajabu kuliko hapo awali.” Faxto aliongeza.
“Wahandisi wa Kanisa la KAG mumebarikiwa, asante kwa mapokezi mazuri." Alitangaza
Maafisa wa upelelezi ambao wamekuwa wakichunguza kifo hicho tatanishi cha Mwathi nyumbani kwa mwimbaji wa Benga DJ Fatxo wanasema hakukuwa na ushahidi wa kimahakama unaoonyesha kwamba marehemu mbunifu wa mapambo aliuawa.
Kulingana na matokeo ya wapelelezi, kutokuwepo kwa Mwathi kuligundulika saa chache baada ya kushindwa kuamka, jambo lililosababisha ukaguzi katika chumba alichokuwa amelala.
Wapelelezi wanaamini Mwathi aliruka kutoka dirishani, jambo ambalo linaweza kueleza ni kwa nini mwili wake uligunduliwa na suruali yake kwenye goti, mara yake ya mwisho kugusa dirisha ilikuwa kiunoni.