(VIDEO)Thee Pluto afichua anavyoendelea baada ya kukiri ana msongo wa mawazo

Alikiri kuwa mitandao ya kijamii si ya watu waliokata tamaa kwa sababu ya wakorofi huku akimpongeza Felicity kwa kuwa mwanamke shupavu.

Muhtasari
  • Hata hivyo, Pluto aliamua kurejea mtandaoni baada ya mashabiki wake wengi kumshawishi hasa kuhusu kushiriki video za majaribio ya uaminifu kwenye YouTube.
Thee Pluto
Image: HISANI

Muunda maudhui na mfanyabiashara  Robert Ndegwa almaarufu Thee Pluto aliwafichulia mashabiki wake muda mfupi uliopita kwamba alikuwa anakabiliwa na msongo wa mawazo na alitaka kupumzika kutoka kwa mitandao ya kijamii.

Aliwaacha mashabiki wakikisia nini inaweza kuwa tatizo lakini hakueleza lolote.

Baadhi ya watu walidhani kuwa huenda alikuwa na matatizo na  mpenziwe na mama wa mtoto wake Felicity Shiru.

Alikanusha madai haya kwenye video huku Felicity akifichua kwamba alitaka tu kupumzika kutoka kwa mitandao ya kijamii ili kutumia wakati mwingi na familia na kuwa karibu na  Mungu.

Kwamba alitaka kupata uzoefu wa jinsi inavyohisi kuishi maisha bila ushawishi wa mitandao ya kijamii na kuwa na wakati mzuri na familia yake na Mungu.

Hata hivyo, Pluto aliamua kurejea mtandaoni baada ya mashabiki wake wengi kumshawishi hasa kuhusu kushiriki video za majaribio ya uaminifu kwenye YouTube.

Alikiri kuwa mitandao ya kijamii si ya watu waliokata tamaa kwa sababu ya wakorofi huku akimpongeza Felicity kwa kuwa mwanamke shupavu.

Siku chache tu baada ya Thee Pluto kubainisha wazi kwamba anaugua kutokana na msongo wa mawazo na kuwataka mashabiki wake kumuombea, mwanablogu Andrew Kibe amedokeza kuwa huenda tatizo hilo ni kutokana na dhana kwamba hajui kama ni baba kweli kwa mtoto Zoey.

Kibe katika podikasti yake ya Jumatatu, alisema kuwa safari hii yuko tayari kumlipa Thee Pluto kiasi cha dola za Kimarekani elfu moja sawa na elfu 135 za Kenya endapo atakubali kufanya DNA na mwanawe Zoey na tukio hilo lirekodiwe naye.

“Thee Pluto kama unasikiliza, niko tayari kufanya hiyo DNA. Acha niiweke hivi, nitakupa dola elfu moja kufanya DNA na pia nitakupa dola zingine elfu moja kwa kukubali tu kufanya DNA,” Kibe alimwambia.

Alimtaka Pluto kukumbatia fursa hiyo na kupata dola elfu moja chini ya dakika kumi ambazo zoezi hilo litachukua.

Hii hapa video ya Thee Pluto akizungumzia anavyoendelea;