logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kama wafuasi wa Yesu! Kwa nini Nicah alikataa posa 12 za ndoa na kumchagua DJ Slahver

Nicah alisema wakati mmoja mama alimchubia kwa niaba ya mvulana wake aliyekuwa nje ya Kenya.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri10 May 2023 - 09:29

Muhtasari


β€’ Pia alidokeza kuwa posa hizo zilikuwa kutoka ndani na nje ya nchi huku kwa kipindi kimoja mama akimchumbia kwa niaba ya mwanawe aliyekuwa nje ya Kenya.

Wapenzi DJ Slahver na Nicah the Queen

Msanii wa injili Nicah The Queen hatimaye amesema ‘ndio’ kwa mpenzi wake wa muda mrefu DJ Slahver baada ya kumvisha pete ya uchumba.

Deejay Slahver alimshangaza mpenzi wake, mwanamuziki wa injili Nicah the Queen, kwa pendekezo lililoandaliwa vyema ambalo aliliandaa kwa usaidizi wa marafiki zao wa karibu.

Katika video hiyo ambayo Nicah aliipakia baadae, Nicah alifunikwa macho na kuongozwa hadi eneo la wazi ambapo Slahver alikuwa chini kwa goti moja, akiwa ameshikilia pete, na binti zake wawili kutoka muungano uliopita walikuwepo.

Hata hivyo, kuvishwa pete hakukuwa gumzo, gumzo lenyewe lilisalia pale kwa kapsheni ambapo Nicah aliandika kwenye video hiyo akitupa dongo kwa aliyekuwa mpenzi wake mcheshi Dr Ofweneke.

Kulingana na Nicah, tangu waachane na mzazi huyo mwenzake, hakupoa kabisa kwani alipata idadi ya wanaume 12 kama wafuasi wa Yesu wakipiga foleni kwake kumposa.

Lakini je, kwa nini aliwakataa wanaume 12 na kumsubiria DJ Slahver tu?

Kulingana naye, posa zilikuwa kutoka ndani na nje ya Kenya lakini alikuwa anahisi kwamba hakuwa amepata mtu sahihi kwake, akidokeza kuwa alikuwa anaongozwa na maono ya Mungu kuhusu yule mtu ambaye atakuwa chaguo mwafaka kuzipa pengo la Ofweneke maishani mwake.

“Tangu nilipotengana na Ofweneke nimepokea posa 12 za ndoa ndani na nje ya nchi na sikuwahi kuwa tayari hadi nilipokutana na SlahverπŸ˜œπŸ’• unapompenda Mungu kuna kitu hutahangaika nacho kama kupata penzi la dhati😜 mama alinichumbia kwa niaba ya mwanae aliyekuwa nje ya nchiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ujinga gani huo!?” Nicha alisema.

Wanandoa hao waligonga vichwa vya habari hivi majuzi walipofichua kuwa uhusiano wao ulikuwa wa useja na kwamba hata wanalala katika vyumba tofauti ili kuepuka vishawishi.

Nicah alisisitiza kwamba anajiokoa kwa ajili ya ndoa, akisema, "Unapofanya ngono nje ya ndoa, unavutia roho nyingi ambazo zinaweza kuwa anguko lako."

Nicah na Dr Ofweneke waliachana mwaka 2017.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved