logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Otile Brown kushiriki 'dinner date' na shabiki 'kienyeji' baada ya marafiki kumdhihaki

Brown alisema akirudi kutoka London atakutana naye kwa chakula cha jioni.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri11 May 2023 - 04:36

Muhtasari


• “Waambie sijali Kach, wewe ni mtu wa ajabu sana na ninakubali upendo wako kwangu" - Brown alisema.

Otile Brown kukutana na Kienyeji aliyechora tattoo yake.

Otile Brown ameahidi kushiriki mtoko wa chakula cha jioni na shabiki wake ‘kienyeji’ baada ya video yake kusambaa akisema anatamani sana kukutana na msanii huyo wa kizazi kipya ambaye hayuko nchini kwa sasa.

Mrembo huyo kwa jina Kach alifanyiwa mahojiano na chaneli ya Mungai Eve na kuonesha matamanio na matumaini makubwa kukutana na Otile lakini alisema marafiki zake walimdhihaki vikali wakimuambia kwamba yeye ni ‘kienyeji’ na kukutana na msanii Otile ni sawa sawa na kujaribu kuvuka bahari kwa miguu peku.

Akijibu mahojiano ya Kach na Mungai Eve, ambapo alikiri kumpenda mwimbaji huyo na kuonyesha tattoo yake ya jina lake, Otile Brown alijitolea kumpeleka nje kwa kahawa akirudi kutoka safari ya London.

Katika video hiyo iliyosambazwa kwenye hadithi zake za Instagram, Kach alikuwa akieleza jinsi marafiki zake walivyomdhihaki kwa kuwa shabiki wa kutupwa na kumpotezea muda mtu ambaye hatawahi kumkubali.

“Wengine walinitusi, waliniambia Otile Brown hawezi taka kienyeji kama wewe, Otile hatakutafuta, unaharibu tu muda wako bure, nikasema tu ni sawa,” Kach alisema.

Otile Brown alikuwa mwepesi wa kujibu, akimwambia Kach asijali marafiki zake na kwamba alithamini upendo na kujitolea kwake.

 “Waambie sijali Kach, wewe ni mtu wa ajabu sana na ninakubali upendo wako kwangu. Kienyeji huwa chenyewe. Kusema kweli nikija tutakuwa na mtoko wa chakula cha jioni na si kukutana kwa kahawa tu,” Brown alisema.

Kach amezidi kuonyesha mapenzi yake kwa Otile Brown, kwani sio tu ana tattoo ya jina lake bali pia ana tattoo ya pili ambayo bado hajaiweka wazi kwa mtu yeyote.

Tatoo ya pili ni ya jina la Otile kifuani mwake, na nyingine ya jina la kimajazi, Obizee, mkononi mwake. Amefikia hata kutumia picha ya Otile kama picha yake ya wasifu kwenye WhatsApp, akionyesha kujitolea kwake kwa mwimbaji huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved