Milly WaJesus afichua sharti pekee litakalomfanya avae pete yake ya ndoa

Sababu kuu ya Milly WaJesus kutoivaa pete yake ni kwamba hapendi mapambo ya bei nafuu.

Muhtasari

• ”Kwa wale wanaoendelea kuniuliza mbona sina pete. Nitaanza kuvaa ile siku @KabiWaJesus atanipatia pete isiyokuwa chini ya $2300.

• Sipendi mapambo ya bei nafuu,” aliandika Milly WaJesus. 

Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Image: Milly Wajesus Instagram

Mwanablogu maarufu Milly WaJesus alifichua kuwa licha ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 5,hapendi kuvaa pete yake ya ndoa aliyonunuliwa na mumewe. 

Milly na Kabi walifunga ndoa mwaka wa 2017 na wakamkaribisha mtoto wao wa kwanza Taji WaJesu mnamo 2019.

Hadithi ya jinsi walivyokutana inavutia sana kwani walipatana kupitia marafiki wao wa karibu.

Kama wanandoa wengine wowote, wamekuwa na changamoto kwa miaka mingi, lakini wamezikumba na kuweza kufanikiwa.

Hata hivyo, Milly yuko kwenye hatihati ya kupata pete yake ya ndoto. Isitoshe sababu yake kuu ya kutovaa pete yoyote ile ni kwamba anaamini kuwa hapendi mapambo ya bei nafuu.

”Kwa wale wanaoendelea kuniuliza mbona sina pete. Nitaanza kuvaa ile siku @KabiWaJesus atanipatia pete isiyokuwa chini ya $2300 . Sipendi mapambo ya bei nafuu,” aliandika kwenye Instastori yake.

Image: Milly WaJesus

Hata hivyo, wanandoa hao walionekana wakitafuta pete ya Milly.