Gumzo pevu Zuchu akilinganishwa na nyota wa zamani RayC, Jaydee na Mdee

Wanamitandao wengine walisema kuwa Zuchu hawezi kufananishwa na Ray C, Vanessa Mdee, na Lady Jaydee kwa sababu yeye ni wa Enzi tofauti.

Muhtasari

• Waliwauliza wafuasi wao kuchagua staa wanayempenda kutoka kwenye orodha na hivyo kuibua mjadala usio na kikomo.

• Wengi waliojiunga na mazungumzo hayo walikuwa na maoni yanayotofautiana huku wengine wakilaumu jukwaa kwa kuwalinganisha.

Hisia mseto zaibuliwa mtandaoni zuchu akilinganishwa na miamba wa zamani wa kike katika muziki wa bongo flava
Hisia mseto zaibuliwa mtandaoni zuchu akilinganishwa na miamba wa zamani wa kike katika muziki wa bongo flava
Image: Instagram

Waimbaji kutoka Tanzania Ray C, Zuchu, Lady Jaydee, na Vanessa Mdee wamekuwa wakitrend kwenye Twitter ya Kenya.

Hii ni baada ya Ripoti ya Wanjiku kuanzisha ulinganisho kati ya waimbaji hao wanne.

Waliwauliza wafuasi wao kuchagua staa wanayempenda kutoka kwenye orodha na hivyo kuibua mjadala usio na mwisho.

Wengi waliojiunga na mazungumzo hayo walikuwa na maoni yanayotofautiana huku wengine wakilaumu jukwaa kwa kuwalinganisha.

Wengine walieleza kuwa  Zuchu hawezi kulinganishwa na Ray C, Vanessa Mdee, na Lady Jaydee kwa sababu yeye ni wa Enzi tofauti na kufanya hivyo kutakuwa ni kukosa heshima kwa waliomtengenezea njia.

Hata hivyo, Wanamtandao wengine hawakukwepa kazi hiyo kwani walimchagua Zuchu kwa urahisi .

Wengine waliegemea upande wa Ray C, na hivyo kumfanya kuvuma kwenye Twitter.

Mashabiki wa kina Lady Jay Dee na Vanessa Mdee hawakuachwa nyuma kwani waliwapa sifa mastaa wanaowapenda.

Maoni kutoka kwa mashabiki:

"Sasa Zuu kafikaje hapo mngemueka hapa Sister P,"  aliandika Rashda Zunde.

"Raycie naye alituroga," ArokoBrivoh aliandika.

"Aaii huyu Ray C naona kila mtu anamtaja ni wa mwaka gani? " Kim aliuliza kwa mshangao.

"Huwezilinganisha prime Ray C na mtu yeyote Bongo," aliandika Emperor Kushnah.

Wanamitandao katika jukwaa hilo walifikia hatua ya kutaja nyimbo wanazozipenda kutoka kwa mastaa wote wanne huku Ray C na Zuchu wakiongoza mbio za kupendwa na mashabiki.