Kiboko yangu-Amberay amlimbikizia mpenziwe sifa tele

Amber Ray ni mwanasosholaiti ambaye amekuwa akijulikana kwa maisha yake ya uchumba, huku Kennedy Rapudo akiwa mpenzi wake wa sasa.

Muhtasari
  • Wiki jana wawili hao walisherehekea mwaka mmoj kwa kuwa pamoja kwa jumbe zenye mahaba tele.
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Kennedy Rapudo na mpenzi wake Amber Ray
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray ameamua kummwagia sifa tele mchumba wake Kennedy kupitia kwa ujumbe wa kipekee.

Alitumia akaunti yake ya Instagram kusambaza picha nzuri na kuandika,

"Leo ninasherehekea mtu huyu hapa ... MCM wangu @kennedyrapudo...yaani kiboko yangu. Nakupenda sana na asante kwa kuwa nguzo yangu,"Aliandika Amberay.

Amber Ray na Kennedy Rapudo wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, na kwa sasa wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Amber Ray ni mwanasosholaiti ambaye amekuwa akijulikana kwa maisha yake ya uchumba, huku Kennedy Rapudo akiwa mpenzi wake wa sasa.

Wawili hao hawajaona haya kuelezana mapenzi na kusifiana kupitia mitandao ya kijamii.

Huku Rapudo akijibu ujumbe wake Amber hakusita kumlimbikizia sifa pia kwa ujumbe wake uliosoma;

"Wewe ni zaidi ya nilivyowahi kutamani, zaidi ya ninavyostahili, na zaidi ya nitakavyowahi kuhitaji. Ninakupenda zaidi na zaidi, kila siku. Ninahisi vizuri sana kuchukua safari hii pamoja nawe jaherana @iam_amberay ❤️,"Rapudo aliandika.

Wiki jana wawili hao walisherehekea mwaka mmoj kwa kuwa pamoja kwa jumbe zenye mahaba tele.

"Tunapojitahidi kupata ukamilifu tunashindwa! Badala yake tunakua pamoja tukijiruhusu kuwa wabichi na wabaya! Kwa njia hii tayari tumekamilika! Tunahoji maisha kwa hivyo tunaishi! Hatuwahi kupigania kipande cha mkate, tunapika pai yetu wenyewe! Hatujisumbui kutafuta kusudi letu, tunazingatia kutumikia kusudi huku tukiwa wazi ili kuruhusu kusudi letu kujitokeza. Upendo ni na upendo utakuwa! Heri ya kumbukumbu ya miaka baba Africanah 🥰 na asante kwa zawadi😇."

Alishiriki video ya chumba kilichopambwa kwa maua, na alionekana kuwa mahali ambapo likizo itakuwa.

Amber Ray alifurahi sana na kumshukuru mchumba wake' kwa ishara yake ya kimapenzi.