Eric Omondi agawa unga wa msaada kwa wakaazi wa Lang'ata

Omondi alishirikisha video akiwagawia wakazi wa Nairobi West unga wa bure kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Muhtasari

• Kwa mara nyingine tena mchekeshaji Eric Omondi ameendeleza huduma yake ya kutoa msaada kwa kuwapa wakazi wa Nairobi Magharibi unga wa bure.

Eric Omondi agawa unga kwa wakaazi wa Langata
Eric Omondi agawa unga kwa wakaazi wa Langata
Image: Screengrab// Youtube

Kwa mara nyingine tena mchekeshaji Eric Omondi ameendeleza huduma yake ya kutoa msaada kwa kuwapa wakaazi wa Lang'ata unga wa bure. Omondi alishirikisha video akiwagawia wakaazi wa Nairobi Magharibi unga wa bure kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika hiyo video Omondi alionekana amefika na gari lililobeba  gunia za unga huku akiamrisha watu waliotaka kugawiwa unga kupanga foleni.

Omondi aliyeonekana kuwa na hasira alikuwa anawaambia wakaazi hao kuwa gari lolote lisipite hapo na iwapo litapita hatawagawia unga.

"Watu wako na mafuta waende huko," alisema kwa hasira.

Omondi ambaye hivi karibuni amedokeza kuacha ucheshi na kuwa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu alidokeza katika ukurasa wake wa Instagram kuwa polisi walizoea sana kuwakamata kila saa ndio walipe dhamana pesa taslimu  ila hiyo siku waliona mchezo wa paka na panya.

Kwani, walifika wakashtuka wamemaliza na kuenda. Aliongezea kwa kusema kuwa jambo ni lazima lifanyike na lifanyike haraka.

Isitoshe alieleza kuwa sukari ambayo ilikuwa shilingi 160 wiki iliyopita ila wiki hii ni shilingi 240, mafuta yamepanda na ushuru uko juu ila wakichukua msimamo hawatafika kwa hivyo, watatoa njia iliyo wazi kwa mwananchi wa kawaida na kusimama.

 

Kitendo hiki kinajiri wiki chache tu baada ya Omondi na wenzake wanne kuachiliwa kwa bondi ya shilingi 20,000 kila mmoja, na dhamana ya pesa taslimu au mbadala wa shilingi 10,000 kila mmoja baada ya mashtaka ya kushiriki katika mkusanyiko usio halali kinyume na Kifungu cha 79 cha Kanuni ya Adhabu.