Rapudo anafanya niseme mapenzi ni kila kitu lakini nikakumbuka bila pesa si kitu - Amber

Amber Ray alishiriki video ya chumba kilichopambwa kwa puto zilizoandikwa "karibu nyumbani mtoto Africanah."

Muhtasari

• Amber Ray alishiriki video ya kukaribishwa nyumbani baada ya kujifungua na mchumba wake Kennedy Rapudo katika ukurasa wake wa Instagram.

Amber Ray na Kennedy Rapudo wamkaribisha mtoto wao wa kike.
Amber Ray na Kennedy Rapudo wamkaribisha mtoto wao wa kike.
Image: HISANI

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray alishiriki video ya kukaribishwa nyumbani baada ya kujifungua na mchumba wake Kennedy Rapudo katika ukurasa wake wa Instagram.

Amber Ray alishiriki video ya chumba kilichopambwa kwa puto zilizoandikwa "karibu nyumbani mtoto Africanah."

Kwenye hiyo video Ray alionekana akikaribishwa katika chumba kilichokuwa kimepambwa kwa rangi za kupendeza na mandhari yenye haiba ya nyota tano na kusema kuwa mapenzi hupendeza zaidi pakiwepo mfuko wenye kina kirefu.

"Weh! Karibu huyu mjaluo anifanye niseme mapenzi ni kila kitu but nimekumbuka bila pesa haingekua hivi 😅….. ," Ray aliandika kwa mbwembwe.

Keki hiyo ilikuwa imeandikwa, "Hongera Amber."

Gavin ambaye ni mwanawe Ray alimkaribisha mamake kwa furaha bashasha na kumpongeza mamake kwa kumpa maua kwani ni dhahiri shahiri kuwa ghulamu huyo amefurahia kupata dad mdogo.

Babake Afrikanah pia alikuwa mwenye furaha sana na kwa hakika  alikuwa wa kumjali mkewe kwani katika ukurasa wake Ray tulimwona Kennedy akiwa na mke wake hospitalini hadi wakati wa kujifungua.

Rapudo na Shicco Waweru(rafiki yake Amber) pia walimpa maua ya kumpongeza Ray na walianza sherehe yao ya kumkaribisha Amber na mwanao Afrikanah nyumbani.

 

Mashabiki wake Ray kwenye mtandao wa Instagram, walimwonyesha mapenzi na kumpongeza kwa kujifungua salama.

"Hongera sana amber ❤️," alimpongeza Ladyrisper na kumalizia kwa emoji za mapenzi.

"Vizuri yako uko Natural😍,wengine wanaenda na mapambo mpaka theater," Hannah.fyp aliandika.