Staa wa Nigeria Seun Kuti akamatwa kwa "kumshambulia polisi"

"Kuti, 40,alinaswa kwenye video akimshambulia afisa wa polisi aliyekuwa amevaa sare," msemaji wa polisi aliongeza.

Muhtasari

• Msemaji wa polisi wa Lagos Benjamin Hundeyin, alitweet kwamba Kuti alijisalimisha siku ya Jumatatu, pamoja na picha ya mwanamuziki huyo akiwa amefungwa pingu.

• Mkuu wa polisi Usman Alkali Baba alikuwa ameamuru azuiliwe siku ya jumamosi.

Msanii Seun Kuti kutoka Nigeria atiwa mbaroni kwa kumpiga polisi
Msanii Seun Kuti kutoka Nigeria atiwa mbaroni kwa kumpiga polisi
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Afrobeat wa Nigeria Seun Kuti amekamatwa kwa madai ya kumshambulia afisa wa polisi.

Msemaji wa polisi wa Lagos Benjamin Hundeyin alitweet kwamba Kuti alijisalimisha siku ya Jumatatu pamoja na picha ya mwanamuziki huyo akiwa amfungwa pingu.

Mkuu wa polisi Usman Alkali Baba alikuwa amamuru kuzuiliwa kwake siku ya Jumamosi.

"Kuti 40, alinaswa kwenye video akimshambulia afisa wa polisi aliyevalia sare,' msemaji wa polisi aliongeza.

Hundyin aliongeza kuwa Kuti ambaye ni mtoto wa mwanzilishi wa Afrobeat, Fela Kuti, alienda katika makao makuu ya polisi Jumatatu na wakili wake na mwakilishi wa familia.

Kabla ya kukamtwa kwake, Kuti alisema kwenye Twitter kwamba polisi huyo alijaribu kumuua yeye na familia yake, lakini hakueleza ni kwa jinsi gani.

Yeye na wakili wake hawajazungumza chochote tangu kukamatwa kwake.

Video zilizochapishwa mtandaoni siku ya Jumamosi zilionyesha wanaume hao wawili wakiwa katikati ya barabara yenye shughuli nyingi ya Lagos.

Haijabainika ni nini kilisababisha ugomvi huo lakini Kuti aliyejawa na hasira alionekana akimsukuma polisi aliyeshangaa kabla ya kumpiga usoni mara mbili.

Mwanamuziki huyo anatweet kwamba atatoa " ushirikiano kamili" kwa uchunguzi wowote.

Kitendo chake kilizua shutuma nyingi kutoka kwa Wanaijeria huku wengi wakitaka akamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka.

Kumpiga kofi afisa wa polisi ni kosa kubwa nchini Nigeria na akishtakiwa na kupatikana na hatia. Anahatarisha kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Kuti ni mtoto wa mwisho wa Fela na anaongoza bendi ya zamani ya Egypt 80 ya babake. Mnamo 2020, alitangaza kufufua chama cha kisasa cha baba yake kilichokufa (Movement of the people) lakini hakuweza kukisajili kwa mamlaka.

Imetafsriwa na Halima Asafa.