Nitaweka rekodi ya Guinneess kama mwanamke mrembo zaidi - Milly Wajesus

Mama huyo wa watoto wawili alivuma mtandaoni kwa 'uchambuzi' wake wa kuvutia.

Muhtasari

• Milly katika siku za hivi karibuni amekuwa mchochezi zaidi katika kauli anazotoa.

Milly Wajesus adai kuwa anaweza kupita kwa urahisi kama mwanamke mrembo zaidi katika rekodi ya dunia ya Guinness
Milly Wajesus adai kuwa anaweza kupita kwa urahisi kama mwanamke mrembo zaidi katika rekodi ya dunia ya Guinness
Image: Instagram

Milly WaJesus anajua sana kuwachokoza Wakenya. Jumanne mama huyo wa watoto wawili alishirikisha wazo la kustaajabisha katika Intastory yake ambalo lilifanya hivyo miongoni mwa Wakenya wengi.

Mwanablogu huyo alianza kwa kuuliza iwapo ataweza kujaribu kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kama Hilda Baci wa Nigeria ambaye aliweza kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kama mpishi aliyetumia muda mrefu sana katika kupika.

"Ninafikiria sana ni rekodi gani ya Dunia ya Guinness ambayo ninapaswa kujaribu kuvunja," aliandika kwenye Instastories yake.

Aliendelea kutafakari ikiwa Wakenya wangemuunga mkono katika azma yake kama vile Wanigeria wamefanya kwa raia wenzao.

"Kweli? Natumai Wakenya wataniunga mkono jinsi Wanigeria walivyomuunga mkono Hilda hadi sote tunamjua sasa."

Lakini hii ilikuwa wakati alipoangusha bomu/mshtuko kwa Wakenya wenzake ambao uliwaacha wengi vinywa wazi.

Na hiyo ilikuwa kwamba angeweza kuvunja Rekodi ya Guinness kwa kuwa mwanamke anayevutia zaidi duniani!

"Anaweza kupita kwa urahisi kama mwanamke mrembo zaidi katika Rekodi ya Dunia ya Guinness," mchochezi alisema.

Maoni yake yalisisitizwa sana huku wanamtandao wakitoa maoni zao kwa ukali katika ukurasa wake wa Instagram.

"Hii sura ahata na make up inakaa kuny'iwa," Thee Ndogogio aliandika.

"Anavutia lakini utu wake umeoza hivyo hata huoni urembo wake," aliandika Elegant  Queen.

"Ashinde ya mwanamke mwenye rohho chafu zaidi Kenya," Dap Labda aliandika.

"Forehead na meno zikiwa wapi," aliandika Alisee Mali."

Hii si mara yake ya kwanza kusema jambo kama hilo linalowashangaza sana mashabiki wake. Wiki chache zilizopita, mke wa Kabi alisema kwa ujasiri kwamba yeye ndiye mke anayependwa zaidi nchini Kenya.

Wakati wa uzinduzi wa kipindi cha uhalisia cha "Oh Sister" Milly alisema kuwa yeye na mume wake ndio wanandoa wanaopendwa zaidi nchini Kenya, huku maombi mengi yakifurika kwenye DM zake kutoka kwa watu wakimwomba awaombee wapate waume kama Kabi.

“Mimi ndiye mke ninayependwa zaidi nchini Kenya. Hii ni kwa sababu ya maombi mengi ninayopata katika DM yangu. Watu wananiambia niwaombee wapate mume kama Kabi. Kabi ndiye mume anayependwa zaidi nchini Kenya,” Milly alisema.