logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwigizaji Dorea Chege apuuza madai ya kuwa mjamzito uvumi wa ujauzito

Maggie, katika Instastory yake alipakia video ambayo ilionyesha kuwa si mjamzito.

image
na

Yanayojiri18 May 2023 - 06:05

Muhtasari


β€’ Dorea Chege almaarufu Maggie, katika Instastory yake alipatkia video ambayo ilionyesha kuwa hana ujauzito.

Dorea Chege

Aliyekuwa mwigizaji katika kipindi cha Maria, Dorea Chege almaarufu Maggie, katika Instastory yake aliweka video ambayo ilionyesha kuwa si mjamzito kwani kwenye video hiyo hakukuwa na dalili yoyote inayoonyesha kuwa yeye ni mjamzito.

Chege katika video aliyopakia alionekana bila mimba ila wiki chache zilizopita alionekana akitomasa tumbo lake lililoonyesha ujauzito uliokomaa.

"Wale wa una ujauzito habari ndio hiyo badooo...." Chege aliandika kwenye Instastory yake.

Dorea alifutilia mbali uvumi uliokuwa umeenea mtandaoni kuwa ana ujauzito.

Wiki chache zilizopita mwigizaji huyo alishiriki video akiwa ameketi kwa furaha akitomasa tumbo lake .

Wanamitandao wachache ambao walifanikiwa kuona kitendo hicho walimpongeza na kumtakia la heri katika safari yake ya ujauzito.

"Hongera sana dear 😍😍 🎊🎊🎊mtoto anafanana na nani ana macho kama nadia mukami,,napenda gym kama babake,,, mimi naimba tu sina maneno πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚" shabiki mmoja aliandika kwa mbwembwe.

Dorea Chege ambaye ni mpenzi wa Dj Dibul ni wapenzi wa kuonesha mahaba yao mitandaoni bila kuogopa huku wakipakia kumbukumbu katika picha wakiwa wanakula bata katika sehemu za kifahari ndani na nje ya Kenya.

Miezi kadhaa iliyopita mpenzi wake Dj Dibul, alikuwa na azimio la kuwania wadhfa wa mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi, azma ambalo halijulikani nini kilitokea na hakuonekana tena kwenye kampeni wala kufika debeni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved