Pesa otas!Eric Omondi avunjisha video akionyesha bunda la pesa huku akimfokea Obinna

Mcheshi huyo alionyesha bunda la pesa ambazo ziliashiriwa kwa maelfu ya pesa za Kenya kutoka chumba chake cha kulia,

Muhtasari
  • Mcheshi huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionyesha mamilioni ya fedha huku akimpa matusi yasiyoweza kuandikwa kwa mcheshi Oga Obinna.
Eric Omondi agawa unga kwa wakaazi wa Langata
Eric Omondi agawa unga kwa wakaazi wa Langata
Image: Screengrab// Youtube

Licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa kote nchini, baadhi ya watu nchini wanaendelea kuonyesha mamilioni ya pesa wanazomiliki,ikiwa ni ndoto ya kila Mkenya kuwa na pesa kutimiza mahitaji yao.

Siku chache baada ya Mike Sonko kuonyesha mamilioni ya pesa, Eric Omondi, mcheshi maarufu pia ametumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kuwaonyesha Wakenya bunda la pesa ambazo anadai ni zake.

Mcheshi huyo aliyeonekana kuwa na hasira alionyesha mamilioni ya fedha huku akimpa matusi yasiyoweza kuandikwa kwa mcheshi Oga Obinna.

Hii ni baada ya mchekeshaji huyo kumtaja Eric Omondi, mlaghai. Awali akijibu kitendo cha Eric Omondi kutoa Unga, Obinna alihoji chanzo cha pesa cha Eric akisema kuwa yeye ni tapeli.

Hili lilimkasirisha Eric Omondi ambaye sasa ametoa video ambapo anaonyesha Mamilioni ya pesa taslimu.

Mcheshi huyo aliyekasirika na kumfokea Obinna kama mtu asiyestahili kuongea naye.

Aidha alidai kuwa yeye nitajiri kuliko mcheshi huyo na kuongeza kuwa anaweza fungua stesheni ya redio na kumwajiri.

Mcheshi huyo alionyesha bunda la pesa ambazo ziliashiriwa kwa maelfu ya pesa za Kenya kutoka chumba chake cha kulia, chumba cha kulala na hata kwenye chumba chake cha kuogea.

Video ya Eric imezua hisia mseto mitandaoni na hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

billymiya: VerifiedYaani celebs kenya ukiudhiwa waachilia zako…acha pia mimi niwachilie zangu in. Few 😂😂😂😂😂

djlyta: KRA nipatieni Kazi...

nasrayusuff: Eric is officially allowed to get 4 wives,and I’m one of them

ynk dollars: Sai oga obinna amekimbia kwa krg kuomba pesa pia yeye arecord 😂😂😂

jamesdenis8: Usikuwe umehire sanduku za sonko we mzee

mbaka casty: I think am the only broke Kenyan...ako si mkona mapesa

pep: Bro me naomba tu unielekezee vle ntapata pesa kama izo. Forever humbled your number one fun❤️