Brenda Otieno, video vixen katika wimbo wa Bahati 'Adhiambo' anadai mwimbaji huyo amlipe kwa kuonekana kwenye video hiyo.
Alitumia mtandao wake wa TikTok kuzungumzia mwimbaji huyo kwa madai ya kukataa ahadi yake ya kuwalipa waigizaji wa video hiyo.
Brenda Otieno alienda kwenye jukwaa lake la TikTok siku ya Jumatano kuelezea kufadhaika kwake, akisema kwamba amekuwa akingoja kwa zaidi ya mwaka mmoja kupokea malipo kutoka kwa Bahati kwa kuonekana kwenye video yake ya muziki.
“Nimechoka kukaa kimya mtu amwambie Bahati nimempa saa 24 anilipe, asiponilipa kwa kuwa video vixen kwenye wimbo wa Adhiambo naenda kumshitaki kwa sababu kuna sheria anachukua faida kwa sababu mimi ni mwanamke video ina views 22m.
Hajawahi kunilipa hadi sasa. Ikiwa hatawasiliana ndani ya saa 24 na kuniambia ni lini atatoa malipo, basi nitamjumuisha wakili wangu katika hili. Sitajiuzulu wakati huu," Brenda alisema.
Kulingana na Brenda, hii haikuwa mara ya kwanza kujitokeza kudai malipo kwa kazi aliyoifanya kwenye video hiyo.
Anasema alinyamazishwa mara ya kwanza alipozungumza lakini safari hii yuko tayari kumchukulia Bahati hatua za kisheria iwapo hatalipwa ndani ya saa 24.
Bahati sasa amezungumzia hayo na kuonekana hajui ugomvi mzima. Ingawa hakuonyesha kama atamlipa au suala hilo linahusu nini, mwanamuziki huyo aliandika kwenye Instagram yake;
"Hii Ngoma imefanya Nini??? So Many Tags🤷♂️🤷♂️🤷♂️ #ADHIAMBO TAZAMA NA KUHESABU MILIONI 22 ZA YOUTUBE!!!"
Wimbo huo maarufu ulitolewa mwaka mmoja uliopita na kuwashirikisha Jaguar na Babu Owino ambao walifanya mwonekano wa kipekee pia.
Baada ya ujumbe wake Bahati, wanamitandao walitoa hisia mseto,na hizi hapa hisia zao;
Dj splash: 22million na 30k ya vixen haulipi mzee😂😂😂😂
Snappy closet: Lipa deni...stop being an user so many complains of you not paying people once they work for you
fitness: Fear kenya women, why is she not involving prince inda na ako kwa song, did bahati call him or the managers , why has she been quiet all that while , was she the only vixen , why are the other vixens not complain , video ilikua hadi na ma mp do you think iyo pesa kidogo ya yeye kupewa ingekosekana tuache kubebwa ufala , this might be a kiki the song is now trending more views more likes, and the lady is also clout chasing , kenyans mtaelewa lini hii industry
ivy: Btw I think huyu dame ni kuclout tu ,,,they were many vixens there na kwanza yeye naeza hesabu mara zenye ameapear kwa screen eti she was athiambo becouse the nyash was nyashing,,,are you the only vixen alikuwa hapo ama wengine walilipwa ukaachwa ,,so ungekosekana hapo hiyo video hatungewatch,,,kweraaaaaaaaaaa🚮