Kifungua mimba ya marehemu Christian Atsu ashinda tuzo ya mchezaji bora

Mjane wa Atsu akipakia picha hizo alisema kwamba maehemu mume wake angekuwa hai angejihisi fahari sana kwa mwanawe kulipeperusha jina la ukoo wake katika kandanda.

Muhtasari

• Mke wa Christian Atsu, Marie-Claire Rupio, alishiriki picha ya mtoto wao akiwa ameshikilia bamba lililopambwa kwa rangi ya fedha na sanduku la zawadi.

• Mchezaji mdogo anayetaka kulipwa alionekana kung'aa alipokuwa akitabasamu kwenye picha

Mtoto wa Atsu ashinda tuzo ya mchezaji bora.
Mtoto wa Atsu ashinda tuzo ya mchezaji bora.
Image: Instagram,

Joshua, mtoto wa kwanza wa marehemu na mchezaji wa zamani wa Newcastle na Chelsea Christain Atsu, alitawazwa kama Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi ya Soka ya Northumberland.

Mke wa Christian Atsu, Marie-Claire Rupio, alishiriki picha ya mtoto wao akiwa ameshikilia bamba lililopambwa kwa rangi ya fedha na sanduku la zawadi.

Mchezaji mdogo anayetaka kulipwa alionekana kung'aa alipokuwa akitabasamu kwenye picha

Akishiriki habari hizo kuu kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Marie-Claire Rupio alibainisha kuwa marehemu babake Joshua angejivunia sana.

Aliandika: Mchezaji bora wa mwaka ⚽️Baba yako angejivunia sana ️

Ujumbe mwingi wa pongezi uliingia kwenye mitandao ya kijamii baada ya watu wengi kuona habari hizo kubwa.

Watu wengi walibaini kuwa marehemu baba yake angejivunia sana kwani wengine walidai kuwa roho yake inaishi kwa mtoto wake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana alifariki kwa ghafla miezi michache iliyopita nchini Uturuki baada ya mtetemeko wa ardhi mbaya Zaidi kukumba taifa hilo.

Atsu alikuwa katika jumba ambalo liliporomoka na shughuli ya kumtafuta ilichukua Zaidi ya siku kumi na baadae akapatikana amefariki.

Wakati wa maziko, mkewe Mreno alifika na kuondoka siku iliyofuata huku watu kutoka taifa hilo wakizua mijadala mitandaoni kwamba hangefaa kuondoka pindi tu baada ya kumzika mume wake kwani katika mila na tamaduni za Kiafrika ni mwiko.

Wengine pia hawakuachwa nyuma walipobaini kwamba hakuna mtoto hata mmoja ambaye alikuwa anamfanana marehemu Atsu.