Fridah Kajala avunja kimya baada ya mwanawe na ex wake kulimana hadharani

Kupitia akaunti yake ya Instagram, alichapisha ujumbe mzito ambao ulionyesha kuwa yuko upande wa bintiye,

Muhtasari
  • Kwa mujibu wa Frida Kajala, Rayvanny ana hatia kwa mambo yote ambayo binti yake alisema, lakini anamlaumu badala yake ili kukidhi ajenda yake.
Kajala, Paula, Marioo
Image: INSTAGRAM

Saa chache baada ya  Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny na Paula Kajala kushiriki vita mtandaoni huku wakirushiana matusi mazito,hatimaye Frida Kajala amevunja ukimya wake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, alichapisha ujumbe mzito ambao ulionyesha kuwa yuko upande wa bintiye, kuhusiana na ugomvi na mwimbaji huyo wa Bongo.

Kwa mujibu wa Frida Kajala, Rayvanny ana hatia kwa mambo yote ambayo binti yake alisema, lakini anamlaumu badala yake ili kukidhi ajenda yake.

"Udanganyifu ni wakati wanakulaumu kwa mwitikio wako kwa tabia yao ya sumu, lakini usiwahi kujadili ukosefu wao wa heshima uliokuchochea," alichapisha.

Wakati wa mzozo wao kwenye Instagram, wasanii hao wawili wa bongo walinyoosheana vidole kuhusu mahusiano yao yaliyovunjika mwaka jana.

Rayvanny ambaye hivi majuzi alirudiana na mzazi mwenzake, Fahyma alidai kwamba binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja alimsaliti kimapenzi na nduguye.

Nilijua unalala na kakangu niliyemheshimu sana kwenye mziki wangu na unajua tunaheshimiana sana, hapo ndipo nilibadilisha mawazo," Rayvanny alisema.

Paula hata hivyo alibainisha kwamba hakuwahi kumsaliti bosi huyo wa Next Level Music wakati wa mahusiano yao ya mwaka mmoja.

Aidha, alidai kuwa mwenzake Rayvanny hata hivyo hakuwa mwaminifu kwani angem'cheat na mzazi mwenzake, Fahyma.

"Nilikaa na wewe mwaka mzima kila mtu anajua tumeachana wakati ulikuwa na mimi na mwanamke wako. Ulitaka niendelee kukaa na wewe wakati unanificha ficha ukienda kwa mwanamke wako unasema nakusumbua, ukija kwangu unasema mwanamke wako anakusumbua," Paula alijibu.

Mwanamitindo huyo wa miaka 20 alimbainishia Rayvanny kuwa alifahamu matendo yake na ndiposa akachukua hatua ya kumuacha.

"Acha kufanya watu waonekane mbaya. Unajua nilijitolea vingapi kwaajili ya haya mahusiano?? Mbona husemi marafiki zangu ulivyolala nao kwenye gari lako," Paula alimuuliza mpenzi huyo wake wa zamani.